Wednesday, September 10, 2008

kikao cha halmashauri kuu ya CCM leo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimu wajumbe wa mkutano wa Halmshauri kuu ya CCM muda mfupi kabla ya kuendesha kikao hicho mjni dodoma leo.Wengine katika meza kuu ni Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume,Katibu mkuu wa CCM Yusuf Makamba na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi taifa akiwmo Waziri kiongozi wa Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha na Mzee John Samuel Malecela wakijiandaa kwa kikao mjini Dodoma
Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa Mzee Kingunge Ngombale Mwiru na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee David Cleopa Msuya wakijadiliana wakati wa Mkutano wa halmashauri kuu ya CCM taifa uliofanyika dodoma leo.
Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Nape Nnauye na Dr Emmanuel Nchimbi wakijadili jambo wakati wa kikao cha Halmashauri kuu ya CCM inayofanyika mjini dodoma leo
shukrani na blog ya michuzi !

No comments: