Tuesday, September 9, 2008

Afande Kova Tupia Macho
Tatizo Hiii....

Pichani Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam(Kanda Maalum)Afande Suleiman Kova akisikiliza kwa makini Malalamiko kutoka kwa mmoja wa wanafunzi waliowakuta kwenye kituo cha mabasi cha mwenge jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya ghafla kituo hapo kuona shida ya usafiri wanayopata wanafunzi jijini Dar es Salaam,pamoja na ziara ya kamanda kova kwenye kituo hicho na vingine bado swala la usafiri jijini Dar es Salaam kwa wanafunzi limezidi kuwa gumu kama muonavyo katika picha hapo chini baadhi ya makondakta wa madaladala wakiwazuia wanafunzi kupanda katika mabasi na wakati mwingine kuwasimamisha nje ya mabasi na kuondoka ghafla bila kuwachukua..

Hii ni kituo cha mabasi kariakoo/Uhuru na MsimbasiBaadhi ya wanafunzi wakigombea usafiri wa kurudi majumbani mwao,Bado watoto wetu wanapata tabu sana kuhusu usafiri wakati wa kwenda shule na kurudi majumbani mwao,Sijui tatizo hili litakoma lini na wahusika bado wako kimya kuhusiana na suala hili.tunaomba afande Kova atupie tena Macho swala hili kwa Vitendo na kuwachulia hatu kali madereza na Makondakta wa mabasi hasa tukizingatia alishajionea Tatizo hili Sugu katika ziara yake kwenye Kituo cha mabasi cha mwenge hivi karibuni.Naomba Kuwasilisha.

No comments: