Friday, December 5, 2008

Uyoga Na Kipilipili!

Labda kuna mahusiano kati ya uyoga na nywele za kipilipili. Tangu utotoni nilipenda sana kula uyoga wa porini kutoka kijijini kwa bibi. Na nywele zangu tangu utotoni ni za kipilipili kama za hao wasichana pichani. Nikizichana haichukui robo saa zimerudi kwenye kipilipili. Na uyoga niliokula nilipenda sana uwekwe pilipili. Na hadi hii leo bado ni mpenzi wa uyoga. Je, kuna watalaam humu ndani wa kutupa ufafanuzi? Pichani ni uyoga wa Iringa. Msimu umeanza, na wa msimu uliopita bado ninao, niliukausha.

No comments: