Huu Ni Ujasiri Au Uwendawazimu?
Picha hii ni ya juma la jana. Bwana huyu nilimkuta akikatisha mbuga ya Mikumi
(pekupeku). Alikuwa akitokea kijiji cha Doma kuelekea Mikumi mjini. Anakatisha mbuga yenye wanyama wakali kama simba na chui. Kuna tembo na mbogo pia. Kuna wanaofanya hivyo kwa kukosa usafiri au nauli, lakini ukikutana anayefanya hivyo na kukataa hata lifti ya gari, basi unahisi kuwa ' ng'ombe' wake ( kichwani) hawajarudi zizini!

No comments:
Post a Comment