Monday, December 15, 2008

Taifa stars wapokewa kishujaa, TASWA yatoa pongezi
kocha marcio maximo akionesha furaha yakemamia ya wakazi wa dar walijitokeza kuipokea stars iliyokuwa katika msafara toka uwanja wa ndege hadi mjini
uzalendo hautushindi tena
baadhi ya wachezaji wa stars wakiwa matumbo wazi baada ya mashabiki kuchukua fulanazzz zao kwa furaha

mkereketwa na mmoja wa viongozi wa kamati ya saidia stars ishinde dk. ramadhani dau naye alikuwepo toka sudan na katika msafara ambapo alidanda juu ya gari toka eapoti hadi mjini
mitaa kibao ilizibwa kwa muda

Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA) tunaipongeza timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Tanzania (Taifa Stars) kwa kufanikiwa kupata tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN) zitakazofanyika Februari mwakani nchini Ivory Coast.

Ushindi wa Taifa Stars ambao iliupata Jumamosi kwenye Uwanja wa Al Hilal jijini Khartoum, Sudan dhidi ya wenyeji Nile Crocodiles umefungua ukurasa mpya wa mpira wa miguu Tanzania kwani ni changamoto kwa michezo mingine kuwa pale ambapo wahusika wanapotimiza majukumu yao ipasavyo hakuna kisichowezekana.

Kwa hatua hiyo mbali ya wadau wengine tunatoa pongezi za pekee kwa wachezaji na benchi lote la ufundi likiongozwa na Marcio Maximo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wadhamini wa timu hiyo Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) na benki ya NMB.

Ni wazi kuwa mafanikio hayo si changamoto kwa wachezaji wa Taifa Stars watakaokwenda Ivory Coast katika fainali hizo zitakazoshirikisha timu nane, bali itakuwa vilevile kwa wachezaji chipukizi na wale wanaoinukia lakini hawafanikiwa kupata nafasi ya kuitwa kwenye timu hiyo.

Pia tunaupongeza uongozi mpya wa TFF uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika Jumapili chini ya Rais Leodegar Tenga na makamu wake wawili Athuman Nyamlani na Ramadhan Nassib.

Uongozi huo una changamoto kubwa ya kulinda mafanikio yaliyopatikana na kutekeleza mengine ambayo hayakufanyika katika awamu iliyopita. Changamoto hiyo ni kubwa kwa vile wadau wana matumaini makubwa kutoka kwa safu hiyo mpya.

Lakini shukrani za pekee ni kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa kuchagua safu ambayo TASWA tuna imani kuwa ina nia, uwezo na sababu ya kukabidhiwa majukumu hayo hasa wakati huu ambapo hamasa katika mpira wa miguu hasa kwa timu ya Taifa imeanza kurudi.
Boniface Wambura
MWENYEKITI




No comments: