Friday, December 12, 2008

globu mpya ya mama na mwana...
Jamani mnasemaje kuhusu watoto kunyonya vidole? Mtoto aachwe aje kuacha tabia hiyo akikua au awe anakatazwa? na nipeni ushauri, akatazwe kwa njia gani, maana mi mwanangu ananipa tabu tabia hiyo.
- Jiang Alipo
-------------------------------------------------------------
Wadau, Mambozzzzzz
Naomba nirushe blog yangu mpya ya
kama jina linavyojionyesha ni blog ya kujipendelea watoto tu!
so wadau nitumieni picha za sherehe mbalimbali za watoto wenu kama b'day, kipaimara, maulidi, ubatizo, hata mtoto akizaliwa namrusha saa hiyohiyo.
tuma picha hizo kwenye:
pia soma upate alimu kuhusu mambo mbalimbali kuhusu watoto na malezihalafu shiriki mijadala na polls mbalimbali: mdahalo wa sasa ni kuhusu watoto kunyonya vidole, na poll ni lini mtoto wa kiume atahiriwe?
karibu u-enjoy!
Love,
Jiang.
----------------------------------
Jiang!
Hongera kwa kujitosa kwenye libeneke la globu. Hakika nimefurahishwa sana kwa uamuzi wako huo wa kuja kivyakovyako, tena kwa mada nyeti ya mama na mwana. Nina imani kabisa kwamba utapata wadau wengi tu, kwani mada na midahalo unayoendesha yanagusa jamii yote.
Karibu sana kilingeni. Natumai hatua hii ya kuigwa italeta changamoto kwa wadau wengine kuanzisha libeneke itayolenga mambo mengine ya maana kama hayo, kuliko wote kuelekeza nguvu kwa habari na matukio.
kadidi !!

No comments: