Saturday, December 20, 2008

Hapa Raha Yake Ni Kwenda Na Ski!


Ndugu Kadidi,
Salaam bwana. Vipi hali ya Dar es salaam sasa? Hapa kama unavyoona, ni barafu kila mahali. Magari hayawezi kwenda kabisa. Hata ofisi kadhaa zimefungwa mjini hapa Eugene, Oregon. Kiasi cha joto cha juu kwa leo asubuhi ni nyuzi 15F, chini ya kiwango cha mgando. Hata maji yanagoma kutoka bombani sababu ya mgando.
Mdau,

Mwipopo, MarkoEugene,
Oregon - USA

No comments: