Tuesday, December 16, 2008

Picha Ya 1986 Ya Makamu Wa Rais TFF Hii Hapa!

Ni Athumani Jumanne Nyamlani ( mwenye suruali nyeupe na kandambili). Niliipiga picha hii mwaka 1986 maeneo ya Veterinari, Temeke kwa Maguluwe. Wa kwanza kushoto ni ' Zicco', anayefuatia nimemsahau jina. Anayemfuatia Nyamlani ni Oswald. Nyamlani na wenzake walikuwamo katika kikosi cha Milla, klabu ya vijana wa eneo hilo la Temeke enzi hizo. Nadhani bado nina picha mbili tatu za wakati huo. Nikipata muda nitapekua katika maboksi yangu na kuzianika maana nilifuatilia sana maendeleo ya klabu ya Milla aliyokuwa akiichezea Nyamlani enzi zake.

No comments: