Friday, December 26, 2008

ALEX GWEBE NYIRENDA, SHUJAA WA MWENGE WA UHURU AZIKWA DAR JUZI
alex gwebe nyirenda jnr. akiwa na picha ya marehemu babu yake na wajina alex gwebe nyirenda juzi kwenye makaburi ya kinondoni ambako shujaa huyu aliyepandisha mwenge wa uhuru kilele cha mlima kilimanjaro amepumzishwa kwenye nyumba yake ya milele katika mazishi ya kifamilia yaliyohudhuriwa na umati mkubwa wa ndugu, jamaa na marafiki katika makaburi ya kinondoni, baada ya misa katika kanisa la mtakatifu columbus.
msalaba wa kaburi la marehemu alex gwebe nyirenda
binti wa marehemu akipewa pole na waombolezaji wakati wa mazishi waombolezaji wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu alex gwebe nyirenda
jeneza likishushwa kaburini
mjane wa marehemu akiweka mchanga kaburini
ndugu jamaa na marafiki wakimzika marehemu alex gwebe nyirenda
sura za huzuni wakati wa mazishi
mjane wa marehemu akiwa na waombolezaji wakati wa mazishi. mbele ni mzee ally sykes nyuma yao ni brigedia jenerali mstaafu hashim mbita
baadhi ya waombolezaji wakisubiri mwili wa marehemu uletwe kwa mazishi. toka shoto ni mzee said el maamry, meja mstaafu kashmir, hamza kasongo, george kritsos na kanali mstaafu julius mbilinyi. alietupa mgongo hakuweza kutambulika mara moja
ANGALIA VIDEO YA SEHEMU YA MAZISHI HAYO KWA
KUBOFYA HAPA

WASIFU WA MAREHEMU ALEX GWEBE NYIRENDA

Nyirenda alizaliwa tarehe 2 Februari 1936 Karonga Malawi, wakati wazazi wake wakiwa katika likizo ndefu ya Krismasi kutoka Tanganyika.
Alisoma shule ya msingi ya Mchikichini Dar- Es-Salaam na baadae shule za Sekondari za wanaume za Malangali (mkoani Iringa) na Tabora, hadi 1957.
Baada ya kuchaguliwa kuendelea na amali ya kijeshi, alijiunga na Chuo cha Kifalme cha Kijeshi cha Sandhurst kama Afisa Kadeti mwaka 1958 na baada ya kufuzu alirejea Tanganyika kujiunga na King’s African Rifles mwaka 1960.
Alipandishwa cheo kuwa Afisa Kamili katika jeshi la wananchi la Tanzania na aliondoka jeshini kama Luteni-Kanali Agosti 1964.
Ilikuwa rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi aliyempa heshima kwa kumpandisha cheo cha Brigadia pamoja na marehemu Brigadia mstaafu Moses nnauye.

Alikuwa Mtanganyika wa kwanza kuhitimu kutoka Chuo cha Kifalme cha Kijeshi cha Sandhurst, akiwa katika kombania ya Waterloo. Alikuwa afisa wa kwanza Mtanganyika katika King’s African Rifles 1960.
Alipewa heshima ya kupandisha bendera ya Tanganyika kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro taRehe 9 Desemba 1961, ambapo wakati huo huo bendera hiyo ilikuwa ikipandishwa Uwanja wa Taifa katika mji mkuu wa taifa jipya la Tanganyika, Dar-es-Salaam.

Brigadia Alexander Donald Gwebe- Nyirenda alikuwa mwanachama wa Rotary Club, mzee wa kanisa la Kipresbiteri la Mtakatifu Kolombas, na mwanachama wa Gideons International.
Alikuwa mcheshi na wote waliomfahamu watamkumbuka kwa hilo. Alikuwa mwanamichezo hodari na alicheza Squash na Golf, mbali na Raga- ambayo aliacha kucheza akiwa na miaka 40- na soka- ambayo aliiacha akiwa na miaka 45!

Brigedia Nyirenda alifariki 20 Desemba 2008 mnamo majira ya saa 12 na dakika arobaini. Ilibainika alikuwa anasumbuliwa na saratani ya umio kutoka Februari 2008; ugonjwa huu ulimdhoofisha hadi alipofariki kutokana na malaria kali.

Alimuoa Hilda Simkoko na walibarikiwa kupata na watoto 5 ambao ni pamoja na Marehemu Alexandra Katie Katinda, Suzyo Maimba Leziya, Atupiye Tima Hope, Alexander Nkutondwa Foti na Tiwonge Buchizga Andrew.

Aidha walikuwa na wajukuu kumi ambao ni marehemu Kanyanta Sampa, Mpumelelo Malumo, Hilda-Katie Miller,Thungo Kuwani
Mkuzom Kuwani, Alexandra Gwebe-Nyirenda, Ethan Gwebe-Nyirenda, Naomi Nkumbula na Jordan Nkumbula.
MOLA AIWEKE MAHALI PEMA PEPONI SHUJAA WETU HUYU
AMINA
UNAWEZA KUSOMA MAHOJIANO YA MWISHO YA MAREHEMU ALEX GWEBE NYIRENDA NA BONGO CELEBRITY KWA

No comments: