Saturday, December 6, 2008

mrema alishitaki jukwaa la wahariri
Kesi ya Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema, dhidi ya wahariri 14 wa vyombo vya habari mbalimbali nchini, itaanza kusikilizwa Machi 3,mwakani, imefahamika.
Kesi hiyo ya madai ya Sh. bilioni mbili itakayosikilizwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ambapo Mrema analalamika kuchafuliwa jina kutokana na ripoti iliyotolewa na Jukwaa la Wahariri.
Akizungumza jana Dar es Salaam, Mrema alisema amewafungulia kesi wahariri hao 14 kama watu binafsi kutokana na kuwa katika ofisi ya Msajili wa Makampuni (BRELA), hakuona majina ya wahariri hao katika usajili wa jukwaa hilo.
Aliwataja wadaiwa katika kesi hiyo itakayosikilizwa na Jaji Razia Sheikh ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Sakina Datoo, Jesse Kwayu, Theofil Makunga, Absalom Kibanda, Muhingo Rweyemamu, Dina Chahali, Saed Kubenea, Jamila Abdallah, Neville Meena na Apolinary Tairo.
Alisema wengine katika kesi hiyo ni Mhariri wa gazeti la Majira, Meneja wa Kampuni ya Uchapishaji ya Business Printers, Mhariri wa Tanzania Daima, na Meneja wa Kiwanda cha uchapishaji cha Printech; na magazeti ya Majira na Tanzania Daima ya Oktoba 15, mwaka huu kwa kutangaza habari za kumkashifu.
Alidai Septemba mwaka huu, Jukwaa la Wahariri lilijipatia jukumu la kufanya uchunguzi wa habari zilizoripotiwa katika msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe na kutoa ripoti iliyomchafulia jina.
Aidha, Mrema alidai kamati hiyo ya uchunguzi kabla ya kutoa ripoti yake ilipaswa kumhoji ili ajieleze kama sheria inavyotaka, lakini cha kushangaza kamati hiyo ilitoa ripoti hiyo bila kumhoji, jambo ambalo amedai amenyimwa haki yake ya asili ya kutakiwa kujieleza na kusikilizwa.
“Habari hiyo imenifedhesha na kunichafulia jina langu hasa ukiangalia mimi ni kiongozi TLP, chama chenye wanachama nchi nzima na wanachama hao wana imani na mimi kiongozi wao, hivyo habari hiyo imenivunjia heshima kwa wanachama, familia yangu na jamii kwa ujumla,” alisema Mrema.
Alisema hata baada ya taarifa hiyo kuchapishwa gazetini aliwataka wadaiwa wote waombe radhi, lakini hawakufanya hivyo, jambo ambalo ameona kwenda mahakamani ili kusafisha jina lake na Watanzania wafahamu ukweli. Oktoba 14, mwaka huu, Jukwaa la Wahariri lilitoa ripoti ya uchunguzi wa Kamati ya Wahariri iliyoongozwa na Kubenea iliyochunguza kuhusu wana habari walivyoripoti msiba wa marehemu

No comments: