Friday, December 12, 2008

aluta kontinyua
Mjadala huu wa Afrika Mashariki hatuwezi kuufunga ama kuuhairisha bila ya kufanya maamuzi yenye manufaa kwa Taifa letu.
Baadhi ya wananchi wenzangu wametoa ushauri na maoni yao juu ya mjadala wawa jumuiya ya Afrika Mashariki. Mjadala huu umepamba moto kwa kasi sana hivi karibuni. Na kumekuwa na kutoelewana katika kufikia muafaka haraka.
Mpinzani wetu mkubwa Kenya, analalamika sana eti kwamba Tanzania tumekuwa kikwazo kwa jumuiya hiyo kufikia makubaliano haraka tusaini mkataba. Hawa Wakenya mbali na kutulaumu kuwa tunachelewesha jumuiya hiyo, utakumbuka kwamba hawa hawa Wakenya ndio waliovunja agano la kwanza, na sasa wanatulazimisha tuingie katika agano jipya bila kufikiria, yaani watuburuze tu!. Haiwezekani hata kidogo.
Hivyo basi, napenda kuchukua nafasi hii kupata maoni ya wazalendo wenzangu, kwani natarajia kutoa kitabu hivi punde Kitakachoitwa MJADAL A WA AFRIKA MASHARIKIHATIMA YA ARDHI YA TANZANIA NA USALAMANimeamua kujitosa katika changamoto hii baada ya kuona kuwa ni sehemu ndogo kati ya watanzania, walio bahatika kutoa maoni yao ama kusoma maoni ya wengine kuhusiana na mjadala huu.
Hivyo basi kudumisha harakati hizi nakusudia kutumia maoni mbalimbali ya wazalendo waliochangia.Katika kuendeleza jitihada za kuilinda Tanzania, nimeazimia kufuta usemi wa jirani zetu kwamba ,eti sisi Watanzania ni watu wa kulalamika tu na hatufanyi chochote cha maana. Hivyo basi, imenilazimu nichukue hatua muafaka kwa wakati muafaka kufuta usemi wao.
Halikadhalika, ninataka kuwatahadharisha umma wa wana wa Afrika Mashariki wajue kuwa, sisi ni kizazi kipya na si cha kudharauliwa, na vile vile kuwahakikishia kuwa hakuna mtu aliyelala usingizi tena hapa Tanzania. Tumesoma, tuna uwezo, upeo na tuko tayari kulinda maslahi yetu na hatima ya taifa letu kwa ajili yetu na vizazi vyetu vijavyo. Kwa hiyo hatuko tayari kukubaliana na masharti haya katika mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Nanukuu, kama ilivyoandikwa kiingereza
Chapter One: common standard travel document" means a passport or any other valid travel document establishing the identity of the holder, issued by or on behalf of the Partner State of which he or she is a citizen and shall also include inter-state passes;
Chapter Seventeen: Free Movement Of Persons, Labour, Services, Right Of Establishment And Residence
Mwisho wa kunukuu
Nisingependa tena kurudia maoni tuliokwisha changia. Kwa kifupi tu wenzetu hasa Kenya na Uganda wana matatizo makubwa sana ya ardhi. Tanzania ndio nchi pekee iliyobaki yenye ardhi kubwa kwa ajili yake na wananchi wake. Daima tunakataa, kwa Tanzania haiwezekani ardhi yetu iporwe.
Kamwe hatuta ruhusu ardhi yetu iporwe,
Sisi ni watanzania halisi,
Raia wa Tanzania,
Watoto wa Tanzania,
Tanzania ndio kwetu.
Baba yetu wa Taifa, MWL. JULIAS K. NYERERE alituambia
Nanukuu
In a country such as this,"... where, generally speaking the Africans are poor and the foreigners are rich, it is quite possible that, within eighty or a hundred years, if the poor African were allowed to sell his land, all the land in Tanganyika would belong to wealthy immigrants, and the local people would be tenants. … but even if there were no rich foreigners in this country, there would emerge rich and clever Tanganyikans. If we allow land to be sold like a robe, within a short period, there would only be a few Africans possessing land in Tanganyika and all the others would be tenants"Mwl. Julius K. Nyerere, 1958
Mwisho wa kunukuu
Ndugu zangu, watanzania tuamke tembeleeni hii website ya Jumuiya hii, na mchimbe kwa makini,
Mwisho, nawapongeza sana viongozi wetu wa sasa, wakiongozwa na Rais wetu, Mh. Jakaya M. Kiwete kwa msimamo waliouonesha kutetea maslahi ya nchi katika mjadala huu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Na pia nawaomba wakumbuke kwamba NGUVU YA UMMA NI KUU, haswa linapokuja suala la kudai haki.
Mungu Ibariki Tanzania
Mwana harakati
Mzalendo halisi
DAR ES SALAAM

No comments: