Saturday, December 6, 2008

boyz ii men waingia mitini.?



Wasanii wa kimataifa wanaotamba sana kwa miondoko laini ya r&b kutoka nchini Marekani, Boyz II Men waliotarajiwa kutua jana mapema asubuhi kwa ajili ya kutumbuiza usiku jana kwenye viwanja vya Lidaz Club hawajafika.

kutokana na taarifa zilizopatikana mapema jana jioni kutoka kwa waandaaji wa onesho hilo ambalo linawajumuisha wasanii wengine kadhaa wa kimataifa akiwemo Joe Lewis Thomas, wameeleza kuwa wasanii hao hawatofika kwenye onesho lao lililofanyika jana usiku kwa sababu ambazo ziko nje ya uwezo wao.
Habari ndiyo hiyo.!

No comments: