Wednesday, December 3, 2008

nimekatwa mguu baada ya harusi


Ebwana katika pita zangu nimeona ombi hili na mimi likantach si kidogo naomba uweke labda kuna wengine litawatach Kuhusu ndugu zetu hawa
Wawili hao ambapo kwa sasa wanaishi eneo la Mbagala Sabasaba, jijini Dar es Salaam walipata ajali hizo kwa nyakati tofauti. Stela alisema mumewe hivi sasa anatembelea magongo.

Akisimulia kwa kina mkasa huo mwishoni mwa wiki iliyopita, Silyvester alisema, mkewe alivujika miguu kutokana na kugongwa na lori aina ya Fuso miezi mitatu iliyopita, wakati yeye aligongwa na pikipiki alipokuwa akitoka kwenye shughuli zake eneo la Magomeni, Mapipa jijini.

"Sipendi kulalamika sana kwani nitakuwa namkosoa Mwenyezi Mungu, mke wangu aligongwa na gari na kusababishwa akatwe miguu yote miwili baada ya kutaka kuvuka barabara, hakuweza kuliona gari hilo lilikuwa likipita kwa mwendo wa kasi, hivyo lilimkanyaga miguuni na kumvuja miguu yote miwili," alisema Geremanus.

Alisema kuwa baada ya ajali hiyo, wasamaria wema walimnyanyua mkewe na kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo alilazwa katika kitengo cha Mifupa (MOI).
Baada ya vipimo vya kutosha, ilionekana kuwa hakuna uwezekano wa kupona, hivyo iliamuriwa akatwe miguu yote miwili.

Hata hivyo, Geremanus alisema kuwa gari lililomgonga halikuweza kupatikana kwani dereva wake alikimbia kwa mwendo wa kasi mara baada ya tukio.

Akizungumzia ajali iliyompata na kumfanya apate kilema cha maisha, Geremanus alisema kuwa alikuwa akitoka katika shughuli zake eneo la Magomeni Mapipa ambapo alikuwa akipita kando ya Barabara ya Morogoro.Alisema akiwa katika enao la karibu na mataa ya kuongozea magari, alishitukia amedondoka chini baada ya kugongwa na pikipiki iliyokuwa ikiendeshwa kwa mwendo wa kasi.

Geremanus alisema kuwa baada ya kupata kilema na mkewe kukatwa miguu yote miwili, wanaishi maisha ya tabu mno kwa kuomba, hivyo anawaomba wasamaria wema pamoja na serikali kwa ujumla kumsaidia kupata fedha ili afanye biashara ikiwa ni pamoja na nauli ya kumrudisha mkewe kijijini kwao, Masasi, mkoani Mtwara.

Kwa wanaoguswa na shida inayowapata wananadoa hawa, wawasiliane nao kupitia simu 0784 937957 .

No comments: