Monday, September 8, 2008

Zain yapanua huduma ya
One Network Saudi
Arabia...
ZAIN,kampuni ya simu inayotoa huduma katika nchi 22 Mashariki ya Kati na Afrika,imepanua wigo wa huduma yake ya One Network katika nchi ya Saudi Arabia,Mashariki ya Kati,ikiwa ni moja ya hatua kubwa zilizopigwa na kampuni hiyo...

Meneja Masoko wa Zain Tanzania, Costantine Magavilla alisema Dar es Salaam kwamba Zain ilianza kutoa huduma hiyo katika Ufalme wa Saudi Arabia wikiendi iliyopita na papo kwa papo ilishuhudiwa huduma ya One Network ikianza Saudi Arabia,nchi yenye miji miwili mitakatifu ya Mecca na Madina.

“Kupanua wigo wa huduma ya One Network kwa Saudi Arabia ni hatua muhimu kwa Zain na hii inadhihirisha tunatekeleza matarajio yetu ya kuwa moja ya kampuni kubwa 10 za mawasiliano ya simu zinazoongoza duniani,na hata kampuni kutoka mabara mengine hazitatuzuia kufanya hivyo,"alisema Magavilla.

"Kutokana na kupanua wigo wa huduma zetu Saudi Arabia,Zain tunadhihirisha tunavyowajibika kwa wateja wetu kwa kutoa huduma bora za simu na kuwarahisishia watu mawasiliano na biashara na shughuli mbalimbali,kitu ambacho ni muhimu kwa Zain katika kutekeleza kauli mbiu ya wonderful world(Ulimwengu Maridhawa),"aliongeza

No comments: