Wednesday, September 10, 2008

Ni Uzembe Ulisababisha Mauaji
Muhimbili – Tume

Waziri wa Afya Profesa David Mwakyusa akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam kuhusu Ripoti ya tume iliyoundwa kutokana na mauaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili yaliyosababishwa na mgonjwa wa akili.
----

Tume iliyoundwa kuchunguza tukio la mgonjwa wa akili kufanya mauaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,imebaini kuwa uzembe ulisababisha tukio hilo na kupendekeza uwekwe ulinzi mahsusi katika wodi za wagonjwa wa akili ili kukabiliana na hatari kama hiyo.


Pendekezo hilo ni moja kati ya mapendekezo matano yalio katika taarifa ya Tume hiyo iliyoundwa mwezi uliopita na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Profesa David Mwakyusa, iliyokabidhi taarifa yake Ijumaa iliyopita ikibainisha chanzo na nini kifanyike kuzuia tukio kama hilo kutokea tena.Bofya na Endelea....>>>>>>

No comments: