Mgomo wa wafanyakazi
Muhimbili Huoo...
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Nchini Bw Wilson Mukama akiongea na Wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo jijini Dar es Salaam ambao wamegoma leo asubuhi nakuvamia ofisi za Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) wakishinikiza kulipwa mishahara mipya, vinginevyo wataitisha mgomo mkubwa ifikapo Jumatatu.Picha hii Kwa Msaada wa Mdau Dr Faustine/SA
----
WAFANYAKAKAZI wa Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH)leo asubuhi waligoma kufanya kazi wodini na kuvamia ofisi za Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya(TUGHE) wakishinikiza kulipwa mishahara mipya,vinginevyo wataitisha mgomo mkubwa ifikapo Jumatatu. Hatua hiyo ilitangazwa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa TUGHE,Bw.Juma Barakabitse,wakati akizungumza na gazeti hili ofisini kwake,huku wafanyakazi hao wakiwa wametaharuki baada ya kutangaziwa kuwa malimbikizo ya nyongeza za mishahara mipya, watalipwa mwishoni mwa mwezi huu.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo,Profesa Leonard Lema,aliwatangazia wafanyakazi hao kuwa mshahara aliopokea kwa ajili ya wafanyakazi wake,haujumuishi malimbikizo bali amepata maelekezo kuwa watalipwa mwezi huu.Huku wafanyakazi wengi wakiwa wametoka sehemu zao za kazi na kuzingira ofisi ya TUGHE na wengine wakiwa wamesimama kwenye makundi madogo madogo,walielezea kusikitishwa na hatua hiyo ya serikali.
Wakati viongozi wa TUGHE wakifanyakazi kuwatuliza,walisikika wakisema wanafanyakazi kwenye mazingira magumu lakini mshahara wanaolipwa ni mdogo.Habari hii na Zamzam Abdul
No comments:
Post a Comment