Wednesday, September 3, 2008

Kesi ya Zombe Yaendelea Kunguruma
Jana:Mahakama Yahamia Eneo
la Tukio...
Wahuhumiwa wa kesi ya Mauaji,wakiwa na wanasheria na Mahakim kwenye
Barabara ya Sam Nujuma jana jijini Dar es Salaam
Shahidi wa 30 katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara,Edson Mmari,akitoa maelezo katika eneo alilodai ndipo walipoawa wafanyabiashara katikati ya Msitu wa Pande ulioko Mbezi Louis jijini Dar es Salaam.Kesi inayowakabili washitakiwa 12 akiwamo mshitakiwa namba moja katika kesi hiyo,Abdallah Zombe,walifikishwa katika maeneo yanakodaiwa kufanyika matukio hayo, ambapo Mahakama iliendeshwa kwenye maeneo hayo kwa muda.Emsom Mmari,ni shahidi wa 30 upande wa serikali.
Watuhumiwa wa kesi ya Mauaji ya wafanya biashara wakipata maelezo
karibu na Ukuta wa Posta
Hali ilivyokua jana Barabara ya sam Nujoma jijini Dar es Salaam pale mahakama Kuu ilipohamia kwa muda eneo hilo kwa ajili ya kusikiliza kesi ya mauaji ya wafanyabiashara inayomkabilia aliyekuwa Mkuu wa upelelezi Kamishana Abdallah Zombe na wenzake ambapo pia ilihamia kwa muda kwenye msitu wa Pande ambako marehemu(wafanyabishara)wanadaiwa kuuawa.Kabla ya kufika kwenye msitu huo Mahakama ilipita pia'ukuta wa posta'eneo ambalo ilidaiwa na askari ndiko yalikofanyika majibishano ya risasi kati ya askari na marehemu.hali ilikuwa tete katika msafari wa kutembelea maeneo hayo yaliyokuwa yakitolewa ushahidi na Mkuu wa Polisi Tabora, Bw.Emsom Mmari,ambaye ni shahidi wa 30 upande wa serikali.Picha hizi kwa msaada wa Dr Faustine na Mdau Yusuf Badi/TSN,kwa mengi juu ya kesi hii Bofya na Endelea Hapa....>>>>>>

No comments: