Monday, September 1, 2008

Ikulu Yatoa Tamko Rasmi juu ya
Hosea na Mwanyika...

Pichani ni Katibu Mkuu Kiongozi Bw Phillemon Luhanjo
--
Na Said Mwishehe na Reuben Kagaruki.
SIKU chache Bungeni taarifa ya Serikali juu ya utekelezaji wa maazimio 23 ya Bunge kufuatia kashfa ya kampuni tata ya Richmond na kubainisha kuwa vigogo kadhaa Serikali waliohusishwa na kashfa hiyo hatIma yao iko ngazi za juu,Ikulu imetoa tamko rasmi.
Miongoni mwa vigogo ambao Bunge liliarifiwa kuwa majaliwa ya ajira zao yako mikononi mwa aidha Rais Jakaya Kikwete mwenyewe au Katibu Kiongozi Ikulu,Bw.Phillemon Luhanjo ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU),Dkt.Edward Hosea,Mwanasheria Mkuu,Bw.Johnson Mwanyika na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Bw.Arthur Mwakapugi.
Ikulu jana imetoa msimamo wake kwa mara ya kwanza juu ya kinachoendelea baada ya kuachiwa dhamana ya uamuzi juu ya vigogo hao.Akizungumza jijini Dar es Salaam,Bw.Luhanjo(Pichani)alisema Serikali haitaki kukurupuka juu ya hatima ya akina Hosea,Mwanyika na Mwakapugi akisema ni suala zito linalogusa maisha ya watu na familia zao.
"Suala hili tunalishughulikia,unaposhughulikia maisha ya mtu haustahili kutoa uamuzi wakukurupuka..tunashughulikia,hatukurupuki,"alisema na kuashiria kuwa kwa sasa kazi iliyoko mbele yao ni kupima uzito na athari za kila uamuzi utakaofanyika Kabla ya kutoa uamuzi lazima upime kwanza na sio kukurupuka..
Hebu fikiria ungekuwa wewe mtu anakuhukumu kufungwa kwa kukurupuka,familia yako na wewe mwenyewe mtaathirika kwa kiasi gani?alihoji.

No comments: