kero ya umeme
Habari ya kazi bwana kadidi2?
Hongera kwa blog yako inasaidia kuelimisha na kuhabarisha watu. Tatizo langu ni moja nakerwa sana na shirika la umeme Tanesco.
Kabla hata hawajatangaza mgao wa umeme sisi wakazi wa Kijitonyama mpakani B tunashida ya umeme kwenye fezi moja na unajua nyumba zetu wengi zina fezi moja tu sio tatu.
Kila wanapokata tumekuwa tunawapigia simu wanasema tunashughulikia eti transfoma ya Queen of Sheba imeelemewa. Sasa kama imeelemewa watafute namna ya kurekebisha.
Lakini kwa kipindi hiki cha hivi karibuni wamezidi maana Jumamosi ya tarehe 4 Octoba 2008 walikata umeme wakaturudishia jumapili asubuhi, jumapili usiku wakakata tena wakarudisha usiku huo huo, jumatatu wakakata wakarudisha jumanne asubuhi, jumanne usiku wakakata tena na kurudisha jumatato asubuhi.
Jumatato usiku wakakata eneo kubwa na kurudisha usiku huo huo. Alhamisi usiku wakakata mpaka sasa navyoandika saa mbili ya asubuhi siku ya ijumaa haujarudi.Naomba msaada wa kuelewa.
Hivi kuna mgao wa usiku siku hizi? Maana kwa wiki tumeshalala giza mara tatu. Ninachoelewa walitangaza mgao wa mchana. Usiku ndio tunahitaji sana umeme sababu ya kiusalama na wengine wanajisomea.
Ni mimi mdau mkereketwa.
Mkazi wa kijitonyama Mpakani B.
No comments:
Post a Comment