Thursday, October 9, 2008

Njia Ya Mchepuko: Ipogolo- Miyomboni
Njia hii ya mkato inapitwa na wananchi wengi wakazi wa vitongoji vya Ipogolo na Kibwabwa wanaokwenda mjini Iringa. Hufanya hivyo badala ya kupanda daladala la Ipogolo kwenda Miyomboni kilipo kituo kikuu cha daladala pale mjini. Hivyo basi, wanabana matumizi ya shilingi mia sita ambazo ni nauli ya kwenda na kurudi. Kutoka Ipogolo kupandisha mjini inachukua takribani nusu saa, wakati wa kuteremsha kurudi Ipogolo ni nusu ya muda huo, kwa maana ya robo saa! Pichani ni daraja la enzi za Great North Road, from Cape to Cairo. Hata wezi wa vyuma chakavu hawajui watumie msumeno gani kukata vyuma hivyo!

No comments: