Thursday, October 2, 2008

chiligati atembelea radio dw ujerumani
Waziri wa ardhi na nyumba ambaye pia ni katibu mwenezi wa ccm Kepteni John Chiligati Akihojiwa na mtangazaji mkongwe Othman Miradji wakati alipotembelea studio za Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani leo. Mh. Chiligati na mheshimiwa Faida Mohamed Bakar mbunge wa mkoa wa kusini pemba walikuwa ziarani hapa Ujerumani. Mh. Chiligati alielezea hamu ya radio Uhuru inayomilikiwa na CCM kushirkiana na DW ili kuisaidia kupata utalaam kutokana na uzoefu ambao DW inao katika masuala ya utangazaji na uandishi wa habari Toka shoto ni Aboubakar Liongo, Mh. Mbunge Faida Bakar, Othman Miraji, Kepteni John Chiligati na Thelma Mwadzaya wakiwa studio za Idhaa ya Kiswahili ya Redio Ujerumani. Asante mdau Mayer Drayer kwa picha mwanana na habari za uhakika toka ulimwenguni kote

No comments: