ANC kumtumia Mbeki katika kampeni Za Uchaguzi Mkuu
Katika hali ambayo haikutarajiwa Chama cha ANC kimesema kuwa kitamtumia aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Bw. Thabo Mbeki katika kampeni za uchaguzi mkuu ujayo. Rais wa Umoja wa Vijana wa Chama hicho, Bw. Julius Malema ametoa kauli hiyo jana usiku, licha ya kuwepo kwa baadhi ya watu ambao wameonyesha kutokuwa na imani na Bw. Mbeki. Bw. Malema ambaye alikua ni kinara wa kumkosoa Bw. Mbeki amesema rais huyo wa zamani bado analojukumu kubwa la kukitumikia chama cha ANC kwenye kampeni.SOURCE: EAR
No comments:
Post a Comment