mambo mswano kwa mtoto samuel nkya
samule kabla ya upasuaji
samuel muda mfupi baada ya upasuaji hospitali ya wockhardt iliyopo mumbai
samuel alivyokuwa baada ya kuvuliwa bandeji
samuel akiandaliwa kwa upasuaji
samuel akiendelea kupata nafuu
nesi akimhudumia samuel
nesi akipiga stori na samuel na nchini ni manesi wanaomhuduma huko mumbai
upasuaji wa kurekebisha sura ya mtoto samuel nkya huko india umefanikiwa na kwa mujibu wa mzazi wake, emmanuel nkya, aliyeongozana naye huko ni kwamba hali yake inaendelea vyema na sura yake sasa inatazamika baada ya kuathirika vibaya sehemu za pua na mdomo.wasamaria wema toka kile pembe walijitokeza kumsaidia samuel mara baada ya globu ya jamii na hii kutangaza matatizo yake na kuomba msaada wa hali a mali. kamati maalumu ikaundwa chini ya mwenyekiti wake david sawe na pia mpiganaji athumani hamisi ambaye naye yuko matibabu sauzi kufuatia ajali ya gari mwezi uliopita. juhudi hizo pamoja na huruma ya wasamaria samuel alifanikiwa kupata pesa za kutosha kwenda india kwa matibabu katikati ya mwezi uliopita.
kwa niaba ya wadau wote, globu hii inampa hongera mtoto samuel kwa kufanikiwa katika matibabu yake huko mumbai, na pia inatoa ahsante kwa wasamaria wema na wadau waliofanikisha zoezi hili kwa michango yao ya hali na mali pamoja na sala.
fuatilia historia yote ya mtoto samuel kwa kubofya hapa
No comments:
Post a Comment