Monday, October 13, 2008

kwa nini hotuba za mwalimu zinabaniwa???
mwalimu julius kambarage nyerere

nimekuwa nikipokea maswali na mamalamiko kibao toka kwa wadau wakitaka kujua sababu kwa nini hotuba za mwalimu nyerere hazipatikani, wakidai kwamba wakienda kuulizia TBC wanaambiwa hazipatikani.

Pia wamelalamika mtindo wa tv na redio kwa kubania hotuba hizo ambapo hutoa kisehemu kiduuuuuchu cha hotuba hizo na kuacha wadau wakiwa na kiu.

Jumanne ijayo ni siku ya Nyerere Day na wadau wengi wana hamu ya kusikia hotuba za muasisi huyu wa taifa hili, lakini jamaa wanabania. wanauliza wadau kwa nini wamatumbi tunakuwa na mawazo ya kiajabu ajabu hata kubania hotuba za mwalimu? wanamwekea nani? kwani zao? hawana haya?

na kila unayemuuliza anakwambia hotuba za mwalimu alizotoa wakati wote wa uhai wake zililenga kipindi hiki hasa, na wanasema kila neno lina maana sana, kiasi cha kumuona huyu mwalimu ni kama nabii.

hii imekaaje wadau?
Napia nawapa pongezi jana kituo cha itv kwa kutupa hotuba ndefu na ilioshiba nikimaanisha ilizungumzia kila kitu ambacho kinatokea kwa sasa hii hotuba aliitoa katika mchakato wa kumchagua mgombea wa urais ambaye kwa wakati huo alikuwa ni mzee wetu Mkapa !!

No comments: