Wednesday, December 31, 2008

Nawatakia Kheri ya mwaka 2009

Mimi kama mmiliki wa hiyi blog nashukuru sana kwa kupita hapa na pia na waahidi kuwa tusubiri mwaka kwa mambo matamu zaidi .
Kadidi !!

Monday, December 29, 2008

kipanya na busara zake !!

ufukwe wa bahari beach

Mtoto mwenye umri kati ya miaka 6-8 akiogelea peke yake
Ufukwe wa Bahari beach ulivyokuwa siku ya sikukuu ya x-mass

wamejaaa kibao uswazi kwetu.!

raha ya mapenzi hujengwa kwa mambo mengi

Raha ilioje kuwa wawili kama hivi pichani mkikatiza kijinjia cha mkato huku mkielekea ufukweni kupunga upepo, tatizo la baadhi yetu mpaka ifike sikukuu ndio tunabebana kwenda huko ufukweni,siku nyingineee aaah WHY .Hata kama hamna kitu ninyi nendeni tu huenda mkaokota

mizinga ya wikend



Saturday, December 27, 2008

Sasa ni Dr Jakaya Mrisho
Kikwete..



Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kenyatta nchini Kenya, Dk.Harris Mule akimtunuku Phd ya Heshima Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa mahafali ya 25 ya chuo hicho yaliyofanyika mjini Nairobi,Kenya SIKU ZA KARIBUNI.Phd hiyo inatokana na jitihada zake za utatuzi wa migogoro kwa nchi za Afrika hasa mgogoro wa Kenya uliozuka baada ya uchaguzi mapema mwaka huu.Picha na Freddy Maro





Jamani pamoja na maboresho ya miundombinu katika sehemu mbalimbali nchini, lakini hii ya sasa ni kali kwa watu wa mbagala afadhari anayetwembea kwa miguuu hufika haraka kuliko kwa gari!

POLISI BWANA HAWAKUWA NYUMA!

Jamaa waliimarisha ulinzi wa kristmas na Mwaka mpya kwa dizaini ya pekee mwaka huu. kikosii maalum kinatumika.
Halafu angani helkopta inazunguka tu kuweka mambo sawa!
A BIG THANK YOU! EVEN IF IT'S STILL EARLY
To each & everyone of you, for the huge impact you had on my life this year…
Especially for all the support & comments I received…
Without you, I'm sure that 2008 would have been extremely boring…
From my side I wish you all a Magical Festive Season filled with ...
Loving Wishes & Beautiful Thoughts…
May 2009 mark the beginning of a Tidal Wave of Love, Happiness & Bright Future…
And to those who need someone special, you are so special stop looking…
To those who need money, LOTTO is back…
To those who need caring, take care of yourselves...
To those who need friends, be careful of backstabbers…
To those who need life, may you find God…
To those who need love, look some more…..Ha! Ha! Ha! Ha! Ha!…
To those who may feel lonely, enjoy it whilst you can…
BUT BASICALLY,
To my friends and loved ones, both old and new…
This is a "THANK YOU" for being there in 2008
…Happy Christmas!!!!!!
and a Prosperous New Year!!!

JAMANI MJIHADHARI


Mshikaji amekamatwa akiwatoa upepo wananchi akijifanya polisi, hii imekuwa noma sasa sijui nani aaminiwe? Ama ndio inatakiwa ukikamatwa ung'ang'anie kwenda kituoni? Jamaa aliingia mkenge akamkamata polisi zikawa arobaini zake. Take care ndugu zanguni!

JAMANI KULA KRISMAS KAZI!

Wasafiri wakisubiri kwenda na treni la bara kula krismas, hakuna hata viti stesheni!
Ubungo tiketi zinauzwa kwa ulanguzi, watu wamegombea mabasi kama daladala!

Wengine walikesha vituoni bado kidogo wasimwone bibi krismas!


Ubungo ilikuwa kazi tupu!



Watu walikuwa wengi wanatamani kula Krismas kwao, lakini najiuliza ni lazima kusafiri kipindi hiki ama ndio zinakuwa ajali za Desemba?

AJALI DESEMBA


Hivi ni kweli ajali kama hizi zinatokea mwezi huu kwa sababu mwisho wa mwak aama kwa sababu ya uzembe!!! Tafakari!
Kipanya na busara zake !!
SALAM ZA MHESHIMIWA BALOZI MWANAIDI SINARE MAAJAR KATIKA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA NOELI NA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA 2009
Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Ireland, Mama Mwanaidi Sinare Maajar, akitoa salam za Noeli na Mwaka Mpya
The Original Comedy, waalikwa wengine na Maofisa wa Ubalozi wakipata Msosi wa pamoja baada ya kupokea salam za Sikukuu ya Noeli na Mwaka mpya toka kwa Mh. Balozi Mwanaidi Sinare Maajar.

Ndugu Watanzania wenzangu,
Kwa mara nyingine tena tumepata fursa ya kufikia kipindi muhimu cha mwisho wa mwaka kwa kusherehekea kwa pamoja sikukuu ya Noeli na kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2009.

Kama ilivyo ada yetu, napenda kujumuika nanyi katika kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa nafasi hiyo.

Kwa niaba ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kwa niaba ya wafanyakazi wenzangu katika Ubalozi wa Tanzania London, na kwa niaba yangu binafsi napenda kuwatakia heri katika kipindi hiki muhimu.

Katika kipindi cha mwaka mmoja Watanzania waliopo Uingereza na Jamhuri ya Ireland wameshuhudia harakati zetu mbalimbali za kuhakikisha wanaimarisha ushirikiano kati yao. Pamoja na kasi ndogo katika harakati hizo, tumeshuhudia mafanikio yaliyotuwezesha kuanzishwa kwa Jumuiya za Watanzania sehemu mbalimbali, zikiwemo Birmingham na Edinburgh.

Huu ni mwanzo mzuri kuelekea kwenye ushirikiano thabiti wa Watanzania waliopo Ughaibuni (Diaspora). Aidha, mwaka 2008 umekuwa na mafanikio makubwa kwa kuweza kufanya Mkutano wa Diaspora hapo Mwezi Aprili.

Mkutano huo ulikuwa na mafanikio makubwa kwanza kwa kuweza kuwakutanisha zaidi ya Watanzania 400, wawakilishi wa kampuni zinazotoa ajira Tanzania na wawekezaji.

Ubalozi wenu unaendelea kufuatilia mapendekezo ya Mkutano huo na kwa kushirikiana na Tanzania Association (TA) tumeshaanza kufikiria kuandaa Mkutano mwingine wa Diaspora kwa kushirikisha washiriki wengi zaidi.

Tunaendelea pia kuwa na azma yenye imani kubwa ya kuwaunganisha Watanzania wote waliopo Ughabuni, si hapa Uingereza na Ireland tu, bali na Ulaya nzima na Amerika.

Tutafanikiwa endapo tutaendelea kuwa na mshikamano thabiti na ushirikiano wa kupigiwa mfano sisi wenyewe kwanza.

Natarajia mtaendelea kusherehekea pamoja fursa hii na kukumbushana kwamba Umoja ni nguvu na siku zote Tanzania itajengwa na Watanzania wenyewe.

Nawatakieni nyote Noeli njema na heri ya Mwaka Mpya.
Mungu Ibariki Afrika,
Mungu Ibariki Tanzania.

BALOZI MWANAIDI SINARE MAAJAR





Friday, December 26, 2008

Kipanya na busara zake !!!!
Mshkaji Anapanda Kijiweni!


Mikumi, jana Alhamisi.
Jamaa Akiwa Peke Yake Ni Wa Kuchunga!
Mikumi, jana alasiri.
Kuna Mawimbi Makubwa Mbele Yake!
Obama akiwa mapumzikoni Hawaii.


Akiila Krismasi!
Akisubiri kuapishwa Januari 20, 2oo9. Ni Barack Obama na bintize.


Kids in school think quickly
TEACHER : Maria, go to the map and find North America.
MARIA : Here it is!
TEACHER : Correct. Now class, who discovered America?
CLASS : Maria!
___________________________________________________________
TEACHER : Why are you late, Frank?
FRANK : Because of the sign.
TEACHER : What sign?
FRANK : The one that says, "School Ahead, Go Slow."
___________________________________________________________

TEACHER: John, why are you doing your math multiplication on the floor?
JOHN : You told me to do it without using tables!
___________________________________________________________

TEACHER : Glenn, how do you spell "crocodile?"
GLENN : K-R-O-K-O-D-A-I-L"
TEACHER : No, that's wrong
GLENN : Maybe it s wrong, but you asked me how I spell it!
___________________________________________________________

TEACHER : Donald, what is the chemical formula for water?
DONALD : H I J K L M N O!!
TEACHER : What are you talking about?
DONALD : Yesterday you said it's H to O!
___________________________________________________________

TEACHER : Winnie, name one important thing we have today that we
didn't have ten years ago.
WINNIE : Me!
___________________________________________________________
TEACHER : Goss, why do you always get so dirty?
GOSS : Well, I'm a lot closer to the ground than you are.

___________________________________________________________
TEACHER : Millie, give me a sentence starting with "I."
MILLIE : I is..
TEACHER : No, Millie.... Always say, "I am."
MILLIE : All right... "I am the ninth letter of the alphabet."
___________________________________________________________
TEACHER : Can anybody give an example of COINCIDENCE?
TINO: Sir, my Mother and Father got married on the same day, same time."
___________________________________________________________

TEACHER: George Washington not only chopped down his father's cherry
tree, but also admitted doing it. Now, Louie, do you know why his father
didn't punish him?"
LOUIS : Because George still had the ax in his hand.
___________________________________________________________
TEACHER : Now, Simon, tell me frankly, do you say prayers before eating?
SIMON : No sir, I don't have to, my Mom is a good cook.
___________________________________________________________

TEACHER : Clyde, your composition on "My Dog" is exactly the same as
your brother's. Did you copy his?
CLYDE : No, teacher, it's the same dog!;
__________________________________________________________
TEACHER : Harold, what do you call a person who keeps on talking when
people are no longer interested?
HAROLD : A teacher.
Mwanamke Mpiganaji

Ethiopia ( Imeletwa na D. Nkya)
Inakuja; Filamu Ya Obama


ALEX GWEBE NYIRENDA, SHUJAA WA MWENGE WA UHURU AZIKWA DAR JUZI
alex gwebe nyirenda jnr. akiwa na picha ya marehemu babu yake na wajina alex gwebe nyirenda juzi kwenye makaburi ya kinondoni ambako shujaa huyu aliyepandisha mwenge wa uhuru kilele cha mlima kilimanjaro amepumzishwa kwenye nyumba yake ya milele katika mazishi ya kifamilia yaliyohudhuriwa na umati mkubwa wa ndugu, jamaa na marafiki katika makaburi ya kinondoni, baada ya misa katika kanisa la mtakatifu columbus.
msalaba wa kaburi la marehemu alex gwebe nyirenda
binti wa marehemu akipewa pole na waombolezaji wakati wa mazishi waombolezaji wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu alex gwebe nyirenda
jeneza likishushwa kaburini
mjane wa marehemu akiweka mchanga kaburini
ndugu jamaa na marafiki wakimzika marehemu alex gwebe nyirenda
sura za huzuni wakati wa mazishi
mjane wa marehemu akiwa na waombolezaji wakati wa mazishi. mbele ni mzee ally sykes nyuma yao ni brigedia jenerali mstaafu hashim mbita
baadhi ya waombolezaji wakisubiri mwili wa marehemu uletwe kwa mazishi. toka shoto ni mzee said el maamry, meja mstaafu kashmir, hamza kasongo, george kritsos na kanali mstaafu julius mbilinyi. alietupa mgongo hakuweza kutambulika mara moja
ANGALIA VIDEO YA SEHEMU YA MAZISHI HAYO KWA
KUBOFYA HAPA

WASIFU WA MAREHEMU ALEX GWEBE NYIRENDA

Nyirenda alizaliwa tarehe 2 Februari 1936 Karonga Malawi, wakati wazazi wake wakiwa katika likizo ndefu ya Krismasi kutoka Tanganyika.
Alisoma shule ya msingi ya Mchikichini Dar- Es-Salaam na baadae shule za Sekondari za wanaume za Malangali (mkoani Iringa) na Tabora, hadi 1957.
Baada ya kuchaguliwa kuendelea na amali ya kijeshi, alijiunga na Chuo cha Kifalme cha Kijeshi cha Sandhurst kama Afisa Kadeti mwaka 1958 na baada ya kufuzu alirejea Tanganyika kujiunga na King’s African Rifles mwaka 1960.
Alipandishwa cheo kuwa Afisa Kamili katika jeshi la wananchi la Tanzania na aliondoka jeshini kama Luteni-Kanali Agosti 1964.
Ilikuwa rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi aliyempa heshima kwa kumpandisha cheo cha Brigadia pamoja na marehemu Brigadia mstaafu Moses nnauye.

Alikuwa Mtanganyika wa kwanza kuhitimu kutoka Chuo cha Kifalme cha Kijeshi cha Sandhurst, akiwa katika kombania ya Waterloo. Alikuwa afisa wa kwanza Mtanganyika katika King’s African Rifles 1960.
Alipewa heshima ya kupandisha bendera ya Tanganyika kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro taRehe 9 Desemba 1961, ambapo wakati huo huo bendera hiyo ilikuwa ikipandishwa Uwanja wa Taifa katika mji mkuu wa taifa jipya la Tanganyika, Dar-es-Salaam.

Brigadia Alexander Donald Gwebe- Nyirenda alikuwa mwanachama wa Rotary Club, mzee wa kanisa la Kipresbiteri la Mtakatifu Kolombas, na mwanachama wa Gideons International.
Alikuwa mcheshi na wote waliomfahamu watamkumbuka kwa hilo. Alikuwa mwanamichezo hodari na alicheza Squash na Golf, mbali na Raga- ambayo aliacha kucheza akiwa na miaka 40- na soka- ambayo aliiacha akiwa na miaka 45!

Brigedia Nyirenda alifariki 20 Desemba 2008 mnamo majira ya saa 12 na dakika arobaini. Ilibainika alikuwa anasumbuliwa na saratani ya umio kutoka Februari 2008; ugonjwa huu ulimdhoofisha hadi alipofariki kutokana na malaria kali.

Alimuoa Hilda Simkoko na walibarikiwa kupata na watoto 5 ambao ni pamoja na Marehemu Alexandra Katie Katinda, Suzyo Maimba Leziya, Atupiye Tima Hope, Alexander Nkutondwa Foti na Tiwonge Buchizga Andrew.

Aidha walikuwa na wajukuu kumi ambao ni marehemu Kanyanta Sampa, Mpumelelo Malumo, Hilda-Katie Miller,Thungo Kuwani
Mkuzom Kuwani, Alexandra Gwebe-Nyirenda, Ethan Gwebe-Nyirenda, Naomi Nkumbula na Jordan Nkumbula.
MOLA AIWEKE MAHALI PEMA PEPONI SHUJAA WETU HUYU
AMINA
UNAWEZA KUSOMA MAHOJIANO YA MWISHO YA MAREHEMU ALEX GWEBE NYIRENDA NA BONGO CELEBRITY KWA

Mambo Ya Krisimasi Kijiji Cha Makumbusho
Jana alasiri alitumbuiza Ndanda Kossovo.
Shamrashamra Za Krisimasi


Mlimani City, jana.
bongo darisalama
Kaka Kadidi,
Bongo raha saaana, ona Hammer na mkokoteni bumper to bumper kwenye foleni, weweeeeeeee
Jana jioni pale Mikocheni mbele ya ofisi za TANESCO jamaa mmoja kaunguliwa na gari. Nilisnepu picha hii wakati ndio kwaaaanza gari la zimamoto linafika. Kama unavyoona moto ulishazimwa na gari la zimamoto limekuja kushangaa tu na kupiga kelele nyingi saaana njiani.
SIKUKUU NJEMA
MDAU

Tuesday, December 23, 2008

taji la miss EA labaki burundi
Miss East Africa, Claudia Nuyimana akivishwa taji katika fainali zilizofanyika wikiendi hii huko Bujumbura, Burundi
MREMBO wa Burundi Claudio Noyimana alijinyakulia gari aina ya Lexus lenye thamani ya zaidi ya sh milioni 40 lililotolewa na kampuni ya Sozmyya Dar es Salaam, baada ya kushinda taji la Miss East Africa.

Katika shindano lililofanyika kwenye hoteli ya Club Di Luc Tanganyika ya mjini hapa, nafasi ya pili ilichukuliwa na Mtanzania, Annete John Mwakaguo wakati nafasi ya tatu ilikwenda Mauritius kwake Anais Veerapraten.

Annete amejinyakulia dola za kimarekani 5000 wakati Anais amejinyakuliadola 3000 huku wote wakipata mkataba wa kufanya kazi na kampuni ya RenaEvents ya Dar es Salaam ambayo ndiyo iliandaa shindano hilo.

Mshindi wa pili Annete Mwakaguo (kushoto) Miss East Africa, Claudio Nuyimana (katikati) na mshindi wa tatu, Anais Veerapatren

tof five kutoka shoto, laura grenouille, rahwa ghidey, anais veerapatren, annete mwakaguo na claudia nuyimana


lynette lwakatare wa tanzania ambaye pamoja na mwenzie aliyetuwakilisha hakuambulia kitu
majaji wakijumlisha maksi za washiriki