Thursday, October 30, 2008

MANJI HATAVUTA WALA NINI, KESHAPONA NA ANAREJEA KESHO TOKA NAIROBI
Julai 2, 2006: Mfadhili mkuu wa yanga yusuf manji akimwaga wino kukubali mkataba wa kuwa mfadhili wa timu hiyo ya jangwani. kulia kwake ni aliyekuwa rais wa yanga wakati huo, francis kifukwe.

HABARI TOKA NAIROBI ZINASEMA KWAMBA MFADHILI MKUU WA YANGA YUSUF MANJI ANAREJEA KESHO AKITOKEA HUKO KWA WATANI WA JADI ALIKOPELEKWA JUZI KWA MATIBABU BAADHA YA KUSHIKWA NA MALARIA KALI MARA TU BAADA YA MECHI NA SIMBA WIKIENDI ILOPITA.


MANJI ALIKIMBIZWA HOSPITALI YA AGA KHAN NA BAADAYE KUPELEKWA NAIROBI KWA CHATA KWA MATIBABU ZAIDI, HALI ILIPOZIDI KUWA MBAYA. HIVI SASA HABARI ZINASEMA KWAMBA HAJAMBO NA YUKO FITI KAMA KAWAIDA YAKE


MTU WA KARIBU SANA SANA NA MANJI AMEIAMBIA GLOBU HII YA inawezekana KWAMBA HABARI ZILIZOTAPAKAA JIJI ZIMA KWAMBA MANJI KAVUTA SI ZA KWELI NA KWAMBA JAMAA ANADUNDA KAMA KAWA.
"UCHOVU PAMOJA NA KUFIKIRIA SANA KABLA YA MECHI NA SIMBA PAMOJA NA FURAHA YA USHINDI BAADA YA UKICHANGANYA NA MALARIA KALI ILIYOMKUTA VIMECHANGIA SANA MANJI KUUGUA GHAFLA.
"HIVI NINAVYOONGEA YUKO ANAPATA LANCHI YAKE NA ANASHANGAA KWA NINI ANAVUMISHIWA KUVUTA WAKATI YEYE YUPO FITI", MTU HUYO WA KARIBU SANA SANA NA MANJI ALISEMA MUDA MFUPI ULIOPITA.
Kipanya na Busara zake...
Kiama Cha Wezi EPA Chawadia

IKIWA imebaki siku moja kabla ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza kiama cha wezi waliochota mapesa katika Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA), kazi iliyokuwa ikifanywa kwa zaidi ya miezi sita na timu ya rais, kufuatilia wizi huo, imekamilika.
Timu hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Edward Hosea, tayari imemaliza kazi hiyo na kupeleka majalada yake kunakohusika kwa hatua zaidi.
Habari ambazo Tanzania Daima imezipata, zinasema kuwa Rais Kikwete ambaye kwa muda mrefu yuko katika ziara za kikazi mikoani, ameamua kulishughulikia suala hilo kwa uhakika ili kurejesha imani ya serikali yake ambayo imekuwa ikipakwa matope kutokana na kashfa hiyo.
Watakaokumbwa na rungu hilo ni wale walioshindwa kurejesha mapesa waliyochota, ambayo ni zaidi ya sh bilioni 133, lakini pia hata wale waliofanikisha uchotaji wa fedha hizo, nao wataguswa.
Vyanzo vyetu vya habari vinadai kuwa Rais Kikwete amepania kuwaonyesha Watanzania kuwa hana mzaha na mafisadi.
Agosti 21 mwaka huu, wakati akilihutubia Bunge mjini Dodoma, Rais Kikwete alisema wazi kuwa wote waliojihusisha na wizi wa fedha za EPA, watachukuliwa hatua kali, ikiwa ni pamoja na kuwaburuza mahakamani.
Aidha, katika hotuba hiyo ambayo Rais Kikwete alisema fedha zitakazorejeshwa zitawanufaisha wakulima, alisema hadi Agosti tayari waliochota fedha hizo walisharejesha zaidi ya sh bilioni 53, huku wengine wakitoa ahadi ya kurejesha zaidi kufikia mwisho wa mwezi huu.
Wezi wa fedha za EPA, waligunduliwa na kampuni ya kimataifa ya ukaguzi wa Ernest & Young, iliyopewa kazi kukagua mahesabu ya BoT na kubaini kuwa fedha hizo ziliibwa katika kipindi cha mwaka 2005/2006.
Baada ya hapo, ndipo rais alipoamua kuunda timu iliyoongozwa na Mwanyika kuchunguza wizi huo.
Habari Kwa Hisani Ya Tanzania Daima

Bosi mmoja wa kampuni ya ujenzi aliamua kutumia nyenzo zake za kazi kulipiza kisasi kwa jamaa aliyempora mpenzi wake.Alipopata nafasi mwafaka ya kulipa kisasi akachukua greda/kijiko na kwenda kupondaponda gari ya "mwizi" wake (hiyo hapo pichani chini).BEWARE!


Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dar es Salaam, wameamua kufunga mageti ya chuo hicho kuzuia uongozi wa chuo kuingia na kutoka baada ya Menejimenti kutotimiza ahadi ya kuongea nao, kutokana na mgogoro wa kufeli kwa wanafunzi wengi katika mitihani yao.



Akipitisha azimio la kufunga mageti hayo, Rais wa Serikali ya Wanafunzi, Ali Mayay, aliwatangazia wanafunzi kuwa magari ya walimu yaliyoko ndani hayatatoka na yaliyoko nje hayataruhusiwa kuingia hadi uongozi wa chuo uzungumze na wanafunzi.



Makamu Mkuu wa Chuo aliyetajwa kwa jina la A. Ahamed, ndiye aliyeahidi kukutana na wanafunzi hao saa nane mchana, lakini hakutokea hali iliyowakasirisha wanafunzi hao na kuanza kufanya fujo. Awali, wanafunzi hao ambao wamegoma kuingia madarasani, walidai kuwa kiini cha wanafunzi wengi kufelishwa ni mgogoro uliopo baina ya Mkuu wa Chuo na walimu wa CBE.



Matokeo ya wanafunzi ambayo yametoka hivi karibuni yanaonyesha kuwa matokeo ni mabaya, hali iliyowashtua wanafunzi wanaotaka kupata maelezo kutoka kwa uongozi wa chuo hicho sababu ya wanafunzi kufeli kiasi hicho. Matokeo hayo ya mitihani yamekuwa mabaya kwa wanafunzi wa jioni waliofanya mitihani ya semista ya tatu pamoja na matokeo ya wanafunzi wanaosoma asubuhi ambao walifanya mitihani ya marudio.



“Sisi tunaamini kuwa mgogoro uliopo baina ya Mkuu wa Chuo na walimu ndio chanzo cha wanafunzi kufelishwa kiasi hiki na sisi tangu Ijumaa tumeamua kutoingia madarasani hadi tupate maelezo kutoka kwa uongozi wa chuo,” alisema Makamu Rais wa Serikali ya Wanafunzi (Cobeso), Godrey Misso. Alisema hawaingii madarasani hadi watakapopata maelekezo kutoka kwa uongozi wa chuo.



“Waliahidi kuongea na sisi jana (Jumatatu), lakini ikashindikana, wameahidi leo (jana) tunawasubiri,” alisema. Alisema haijawahi kutokea katika historia ya chuo hicho wanafunzi kufeli kiasi hicho. “Haiwezekani katika darasa la watu 400 wafaulu watu sita, ina maana wanafunzi wengine hawana akili?…hiki ndicho tunachopinga,” alisema. Baadhi ya walimu waliozungumza na gazeti hili, walikiri kuwa Mkuu wa Chuo hicho, Dk. Wilclif Lugoe tangu ajiunge na chuo hicho miezi 10 iliyopita, amefanya marekebisho ya mfumo wa uendeshaji ambayo yanawaathiri walimu kimapato.

WASTAAFU EAC WAZUA JAMBO!

Baada ya kuingia mtaaani wazee hao walionja mabomu ya mchozi.
Gari la Polisi wa FFUlikiwanyunyizia dawa ya macho na mapafu wazee hao.
Mkuu wa Mkoa, Abbas Kandoro, akiweka mkakati wa kuwafanyizia wazee hao na Kamanda wa Kanda ya dar es Salaam, Suleyman Kova.

Mmoja wa wazee hao akomwaga radhi!
Walianza wakiwa tuli barabarani hawakujua ambacho kingefuatia.

VIONGOZI wa serikali, wafanyabiashara wakubwa, mabalozi na wananchi wa kawaida jana walionjeshwa ukubwa wa machungu wanayopata wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wakati wazee hao walipoweka kizuizi katika eneo la daraja la Sarenda na kusababisha magari kushindwa kuingia katikati ya jiji.
Eneo hilo, lililoko makutano ya Barabara ya Ali Hassan Mwinyi na Umoja wa Mataifa, ambako kuna kituo cha polisi cha Sarenda, ndio njia kuu na pekee ya magari yote kutoka maeneo ya Oysterbay, Mikocheni, Msasani na Ada, ambako wanaishi viongozi na watendaji wakuu wa serikali, mabalozi na maofisa wengine wa taasisi za kimataifa hupitia.
Maeneo ya Kinondoni, Mwenge, Kawe, Tegeta na Mbezi ambako wanaishi wananchi wa kipato cha chini na kati, pia waliathirika na mbinu hiyo ya wastaafu wa EAC kuishinikiza serikali kuwalipa mafao yao baada ya jumuiya hiyo kuvunjika mwaka 1977.
Na kutokana na maeneo hayo kuishi vigogo wengi, msururu uliozuiwa ulikithiri 'foleni' za kawaida na kusababisha watu wengi kuchelewa makazini.
Wastaafu hao wanaokaribia 200 wanataka serikali iwalipe madai yao ya fedha ambazo wanadai, ambazo ni jumla ya Sh300 bilioni.
Katika kikao chao cha juzi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, wastaafu hao walidai kuwa wangeamkia ubalozi wa Uingereza ambako walidai wangepiga kambi hadi suala lao litakapopatiwa ufumbuzi.
Lakini kiongozi wao, Nathaniel Mlaki akaeleza kuwa kabla ya kwenda ubalozini, wangepitia sehemu moja, ambayo hakutaka kuitaja na kuwahimiza wenzake kuwahi asubuhi ya jana ili waelezwe sehemu hiyo na kuwataka wabebe chupa za maji.
Baada ya kufika katika eneo hilo saa 12:20, wastaafu walilala barabarani huku wakisema maneno mbalimbali ya kuilaumu serikali kabla ya kuvua nguo baadhi yao, alisema shuhuda mmoja aliyekuwa eneo hilo wakati wa tukio.
Kutokana na hali hiyo magari yote yanayotumia barabara hizo yalikwama kwa muda wa zaidi ya saa mbili na nusu kabla ya wastaafu hao kuondolewa kwa nguvu na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).
habari na mzee wa sumo !!

Jamani kazi nyingine ngumu! Hebu cheki hawa vijana walivyombeba mzee huyu utafikiri mtuhumiwa wa EPA kapatikana!?

Hebu nipeni Kepsheni ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Mbunge wa Longido Lekule Laizer walipokuwa wakizungumza bungeni. mimi sijui!!!
Ujumbe
Umeletwa na Kau Mose.
AU Yawabana Viongozi Wasiotii Demokrasia

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Rais Jakaya Kikwete, amesema umoja huo hautawavumilia viongozi wanaoingia madarakani kwa njia zisizo za kidemokrasia. Amesema nchi za Afrika lazima ziheshimu na kulea njia ya kidemokrasia katika kupata viongozi wake. Rais Kikwete alisema hayo juzi alipofungua rasmi kikao cha 10 cha Bunge la Afrika, kwenye ukumbi wa Bunge hilo ulioko Midrand mjini hapa. “Msimamo wa zamani wa kutoingilia mambo ya ndani ya nchi mwanachama hauna nafasi tena katika bara letu. Afrika sasa haiwezi kuendelea kukaa pembeni na kuangalia maadili ya kidemokrasia yakivunjwa, au serikali inapokandamiza raia wake,” alisema na kusisitiza kuwa ni lazima AU ichukue hatua dhidi ya tawala za aina hiyo. Alisema bara la Afrika siyo tena bara la kuendekeza utawala zisizoheshimu demokrasia, haki za binadamu na utawala wa sheria, na ni muhimu suala la kupata viongozi wake kwa njia za demokrasia ziheshimiwa na kulinda. “Serikali yoyote itakayoingia madarakani kwa njia zisizo za kidemokrasia haitakubalika na itasimamishwa uanachama wake kwenye Umoja wa Afrika. Uamuzi huu umeshaanza kutekelezwa kwa baadhi ya nchi (ambazo viongozi wake wamejitwalia madaraka), Mauritania ikiwa mfano wa karibu,” alisema.
Alisema Afrika ni lazima ilinde misingi ya kidemokrasia, utawala wa sheria na haki za binadamu zinazoonekana sasa katika bara hilo kwa kuheshimu uchaguzi wa kidemokrasia na matokeo yake. Utamaduni wa nchi kufanya uchaguzi muda unapofika, alisema umeimarika na kutekelezwa na nchi kadhaa za Afrika, akisema tangu kuanzishwa kwa Bunge la Afrika mwaka 2004, uchaguzi wa kidemokrasia na wa wazi umefanywa katika nchi 45; mwaka pekee nchi tano zimefanya uchaguzi. Alisema wakati Afrika inafurahia maendeleo hayo ya kidemokrasia, bado kuna matukio machache yasiyofurahisha, na amelitaka Bunge la Afrika kuunga mkono juhudi za kulinda demokrasia, haki za binadamu na utawala wa sheria.
Rais Kikwete amesema analitarajia Bunge hilo kuwa chachu na nguvu ya kulinda misingi hiyo, kwa kujadili na kuwasukuma viongozi wa Afrika juu wa wajibu wao wa kuheshimu utawala bora, kulinda haki za binadamu na kuwajibika kuhakikisha utawala wa sheria katika nchi wanazoziongoza. Mapema akimkaribisha Rais Kikwete kufungua kikao hicho cha Bunge, Rais wa Bunge hilo, Balozi Getrude Mongela, alisema lina wabunge 245 kutoka nchi 47 zinazowakilishwa.
Habari Kwa
Hisani Ya HabariLeo
Ali Kiba Adatisha Wadau
Atlanta ......
Pichani ni mwanamuziki kutoka Bongo Ali Kiba akibagawisha wadau mbalimbali kwenye show yake ya kufa mtu nchini marekani mjini wa Atlanta

Wednesday, October 29, 2008

KP NA BUSARA ZAKE....

wastaafu wafunga barabara dar kudai mafao yao
mpaka kieleweke...
Hi Kaka Kadidi,
Leo nilibahatika kuwahi katika kiunga cha barabara za Ali hassani mwinyi na Umoja wa mataifa kwenye mataa ya salenda karibu na kituo kidogo cha polisi ambapo wazee wa iliyokuwa EAC walikaa katikati ya barabara na kusabisha foleni kubwa na magari kutokwenda mjini.
Ilikuwa milango ya saa moja kasoro hivi wakilisha kwenye Globu yetu ya inawezekana wadau waone hii.Wazee wanadai mafao kwa miaka thelathini sasa.
Mdau fisi kubwa

MAANDAMANO YA WANAHABARI








Picha zote kutoka Jamiiforums

Tuesday, October 28, 2008

hivyo ndivyo fiesta ilivyofana dodoma

Nyuma ya jukwaa pia kushoo love kulikuwepo na kubadilishana mawazo kimtindo kama hivi kwa kutosha kabisa.Toka shoto ni albert Mangwea, Mhariri wa gazeti la Mwananchi starehe Henry Mdimu a.k.a Zee la Nyeti pamaja na Mwana-FA
Mh Temba kutoka kundi la wanaume TMK akiwakilisha vilivyo jukwaani,

Baadhi yao walijiramba mpaka kupitiliza kama uoanavyo pichani,jamaa alijiramba mpaka ile akhaaa! si umecheki kopo zake mbili pembeni za naniihiiiii hana hamau nazo tena


Prof Jay nae kama kawa na umahiri wake wa kuieteka hadhira vilivyo ndani ya uwanja wa Jamuhuri Dodoma jana jioni




Mwana-Fa akizikonga nyoyo za wakazi wa Dodoma jana jioni kwenye tamasha la fiesta jirambe,ambapo maelfu ya mkoa huo walijitokeza kujionea live bila chenga wasanii wawapendao .Washikaji baada ya kumaliza Dodoma, libeneke linaendelezwa jijini Mwanza .a.k.a The Rock City,ambako fiesta imepangwa kufanyika usiku wa jumamosi a.k.a Novemba1 katika ukumbi wa Yatch Club na Jumapili ngoma inahamishiwa uwanjani CCM kirumba huko ndiyo washabiki na wapenzi wa fiesta wanapewa nafasi kubwa ya kujiramba kwa nafasi kabisa.Si ya kukosa babake,yaani full mizuka

Msanii kutoka nyumba ya vipaji (THT) Mwasiti akilivua pendo mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa Dodoma waliofika jana jioni kwenye tamasha la fiesta
Wakazi wa Dom walijitokeza kwa wingi kuunga mkono tamasha la fiesta jirambe lililofanyika jana mchana ndani ya uwanja wa jamhuri

Jay Mo akighani huku umati wa wakazi wa Dom ukimsilikiza kwa makini


Ukipenda muite brazamen au Mr Misifa Dully Sykes akionesha umahiri wake wa kucheza na maik mbele ya umati wa wakazi wa Dom hiyo jana jioni



Wasanii kutoka nyumba yenye vipaji a.k.a THT wakiwa jukwaani wakiwakuna wakazi wa Dodoma jana mchana kwenye tamasha la fiesta jirambe lililofanyika kwenye uwanja wa mpira wa Jamhuri,ambao maelfu ya wakazi wa mji huo walijiachia vya kutosha



Vibweka kama hivi vya kujiachia kutoka juu ya jukwaa vilikuwepo vya kutosha tu,na watu walipata rahaaa

Ilikuwa ni full kujiramba,mayowe,shangwe zilipata mahala pake,kila shabiki alieonekana kukunwa vilivyo na msanii yeyote yule hakusita kupiga winja na kuinua mikono hewani



Tamasha la fiesta jirambe 2008 jana mchana lilikuwa pande ya wakazi wa Dodoma,eebwanae ilikuwa ni noma,wakazi wa Dodoma wanajua kujiramba ile kisawa sawa,jana jirambe ilikuwa inafanyika ndani ya uwanja wa mpira wa Jamhuri,wasanii wa chini ya handaki walianza kupanda jukwaani kuanzia majira ya saa sita na ushee hivi na baadaye wakongwe waakaanza kuangusha libeneke la bandika bandua,palikuwa hapatoshi uwanjani hapo.Pichani ndio kama uonavyo umati wa wakazi wa Dodoma ulivyoamua kujiramba kwa staili ya aina yake.

WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI WAANDAMANA

mimi katika picha hizi uliponitumia sikuzielewa mkuu nashukuru kwa picha kumbe maana yake wamezibwa mdomoi poleni jamani !!


Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari wakiwa kwenye jengo la Wizara ya habari,Utamaduni na Michezo baada kufanya maandamano leo asubuhi kuanzia mtaa wa Lugoda jijini Dar na kufikia wizarani hapo kwa Mh George Mkuchika na kuacha barua iliobeba ujumbe mzito,huku wakiwa wamefunga midomo yao na plasta kupinga kitendo cha Serikali kulifungia kwa muda wa miezi mitatu gazeti la Mwana halisi na pia kuishinikiza irekebishe sheria ya uhuru wa vyombo vya habari ya mwaka 1976.
OBAMA ASSASSINATION PLOT FOILED


WASHINGTON — Federal agents have broken up a plot to assassinate Democratic presidential candidate Barack Obama and shoot or decapitate 102 black people in a Tennessee murder spree, the ATF said Monday.

In court records unsealed Monday, federal agents said they disrupted plans to rob a gun store and target a predominantly African-American high school by two neo-Nazi skinheads. Agents said the skinheads did not identify the school by name.

Jim Cavanaugh, special agent in charge of the Nashville field office for the Bureau of Alcohol, Tobacco, Firearms and Explosives, said the two men planned to shoot 88 black people and decapitate another 14. The numbers 88 and 14 are symbolic in the white supremacist community.

The men also sought to go on a national killing spree, with Obama as its final target, Cavanaugh told The Associated Press.

"They said that would be their last, final act _ that they would attempt to kill Sen. Obama," Cavanaugh said. "They didn't believe they would be able to do it, but that they would get killed trying."
Heshima Hela

Heshima hela, haya ndio maneno yaliyopo nyuma ya baiskeli hii maarufu kama Guta. Kijana anafanya kazi apate fedha aweze kuheshimika mtaani.

Mambo ya upimaji wa macho !!


Vipimo vya macho hivyo. mama huyu mkazi wa Kisarawe mkoani Pwani akipima macho yake kwa ajili ya kupatiwa tiba.
kikao cha kumi cha bunge la africa
mbunge wa kisarawe ambaye pia ni mbunge wa afrika mh. athumani janguo (pili shoto) akishiriki katika kikao cha 10 cha kawaida cha bunge la afrika jana huko pretoria baada ya kufunguliwa na mwenyekiti wa umoja wa afrika JK
jk atua sauzi kuzindua
JK akipokewa na Rais wa Bunge la Afrika Dk. Getrude Mongela uwanja wa ndege wa Oliver Tambo usiku kuamkia jana. Mchana huu Jk amefungua kikao cha 10 cha kawaida cha bunge hilo na kurejea bongo kuendelea na ziara yake ya siku 8 ya mkoa wa tabora

Maria Namiiro Ni Mtanzania?

Ndugu kadidi2
habari za kazi? pole na mishughuliko.
Naomba tusaidiane .katika blog yetu alitokea binti ambaye eti kaiwakilisha Tanzania katika FACE OF THE UNIVERSE iliyofanyika nchini GHANA hivi karibuni. lakini kiukweli binti huyu sio mtanzania. ona mwenyewe. BLOG YETU YA JUMUIYA YA WATANZANIA ITALY NI: http://www.tnzncommunity.blogspot.com

Face of the Universe


Maria Namiiro
Osagyefuo Amotia ofori panin Okyenhene The King and Queen Mother
MARIA ALIPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA NCHINI GHANA KATIKA ''FACE OF THE UNIVERSE.

WADAU KAMA MNAKUMBUKA BINTI HUYU NILIMTOA KATIKA BLOG HII KUWA KAIWAKILISHA TANZANIA KATIKA "FACE OF THE UNIVERSE" ILIYOFANYIKA GHANA. NILIPATA MAIL YAKE NA KUMUUANDIKIA KUMPA PONGEZI,LAKINI JIBU LIKAJA KUWA HAJUI KISWAHILI!!! NDIPO NIKAMUULIZA INAKUWAJE HUJUI KISWAHILI? AKAJIBU KUWA BABA YAKE NI MTANZANIA NA MAMA YAKE NI RAIA WA UGANDA.NIKAMUULIZA YEYE NI RAIA WA WAPI? AKAJIBU KUWA YEYE SIO MTANZANIA WALA MGANDA ,YEYE NI BRITISH CITIZEN! SASA WADAU INAKUWAJE RAIA WA NCHI NYINGINE AKACHUKUA NAFASI AMBAYO TUNGEWAKILISHWA NA MTANZANIA WA KWELI.NI KWAMBA BINTI HUYU ANATUMIA JINA LA TANZANIA KWA FAIDA ZAKE BINAFSI. TUNAOMBA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA AMBAKO NDIO ANAISHI BINTI HUYU,WAPATE MAELEZO JUU YA JAMBO HILI KWANI NIONAVYO MIMI NI MAKOSA KUPEPERUSHA BENDERA YA NCHI NYINGINE KWA KUDANGANYA KUWA WEWE NI RAIA KUMBE SIO. KAMA NINAKOSEA BASI NAOMBA NIPEWE MAELEZO ZAIDI ILI NA MIMI NIELEWE. NA KAMA MARIA NAMIIRO UNA MAELEZO YOYOTE TUNAOMBA UTUFAHAMISHE.