Friday, May 2, 2008

Rostam Taabani !!!

Na mwandishi wetu.
Mwanahalisi.

Mbunge wa Igunga (CCM), Rostam Aziz, ametishia kujiuzulu ubunge kutokana na hatua ya kamati ya Uongozi ya bunge kumzuia kuwasilisha hoya yake bungeni, Mwanahalisi limedokezwa.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya kamati hiyo, zinasema Rostam alitoa tishio hilo mbele ya wajumbe wa kamati ya uongozi ambao pamoja na Spika wa bunge, Samweli Sitta na Waziri mkuu Mizengo Pinda.

Inaelezwa kwamba baada ya Rostam kutoa kauli hiyo, Waziri Mkuu na Spika pamoja walimtaka afanye hivyo haraka.

"Kabla rostam hajamaliza kulalama, Spika hakumkawiza. Alisema, "Andika barua ya kujiuzulu sasa hivi. Hatuwezi kupeleka matusi haya ndani ya Bunge....." alinukuliwa na mjumbe mmoja wa Kamati.

Mjumbe huyo alisema kauli ya Rostam iliwaudhi wajumbe wa Kamati ya Uongozi kwani haraka Waziri Mkuu alitoa tamko la kuungana na Spika Sitta kumtaka Rostam ajiuzulu ubunge.

wiki iliyopita, Spika alimzuia Rostam kuwasilisha maelezo yake bungeni, baada ya kubaini kuwa aliyoyaeleza katika kile alichoita "Hoja yake" hayakustahili kuwasilishwa bungeni.

Katika Mkutano wa bunge uliopita (wa kumi) bunge lilimtaka Rostam kuwasilisha maelezo yake katika mkutano unaolendelea sasa mjini Dodoma, baada ya kusikika akituhumu kwamba kamati teule ya Bunge iliyochunguza mkataba wa Richmond, " aliendelea na kazi zake hata baada ya kuwasilisha ripoti yake kwa Spika"
Rostam kwa mujibu wa taarifa yake kwa spika.

Rostam kwa mujibu wa taarifa alitaka Spika kwa kutumia hoja za Rostam , amwamuru Dr. Mwakyembe kumsafisha ndani ya bunge.

Hata hivyo shinikizo lake hilo lilikataliwa na kamati ya Uongozi.

Taarifa za ndani ya bunge zimesema kukataliwa kwa maelezo binafsi ya rostam kumetokana na konekana yamejaa tuhuma, shutuma na dharau kwa bunge na kamati teule ya Mwakyembe.

Spika wa Bunge amekiri kupokea hoja binafsi ya Rostam, lakini alisema ameshindwa kuruhusu iwasilishwe bungeni kutokana ka kwend kinyume na kanuni za bunge.

Mjumbe mmoja wa Kamati ya uongozi amemkariri Spika akisema Bunge halikujadili hoja ya Rostam, siyo kwa kumwogopa, kama baadhi ya magazeti yanavyotaka kuonyesha, bali kwa sababu hoja yenyewe inakiuka kanuni za Bunge.

Alipopigiwa simu na gazeti hili kupata undani wa taarifa hiyo, Sitta aliekeza mwandishi awasiliane na Rostam mwenyewe ambaye Spika alisema tayari amejulishwa uamuzi huo.

Mwanahalisi halikuweza kuwasiliana na Rostam kupata upande wake.

Katibu wa wa wabunge wa CCM, alli Ameir Mohammed, alipoulizwa juu ya suala hili alisema, "sijui kilichojajiliwa. Sifahamu kamati ya Uongozi wa wabunge wamesema nini. Sikuwepo Dodoma na wala sijakutana na mwenyekiti wangu, wala Rostam"

Hata hivyo, imefahamika kuwa wajumbe wa kamati teule walikuwa wamejiandaa vilivyo kulithibitishia taifa kuwa Rostam ndiye mwenye Richmond na Dowans.

Uchunguzi wa Mwanahalisi umeonyesha kuwa wajumbe walikuwa wamekamilisha kile kilichoitwa misumari ya mwisho wa kumpigilia Rostam.

Wiki iliyopita Rostam alimweleza spika wa bunge, nia yake ya kutoa maelezo binafsi kuhusu madai ya kamati teule kuwa ilihuka na njama za kufisadi za kuibeba Richmond.

Taarifa za Bunge zimesema hakukubaliwa kw amujibu wa kanuni za 53(8) na 54(4) za kanuni za kudumu za bunge, toleo la 2007 zinazopinga kuwa "Mbunge yeyote hataruhusiwa kufufua jambo lolote ambalo bunge lilikwisha kuliamua ama katika mkutano huo au ule uliotangulia.

Imefahamika kuwa Rostam katika hoja iliyokataliwa na Spika, aliwaita wabunge kuwa ni wasanii na wababaishaji kwa babau tu walimshuku kwenye taarifa yao kuhusika na mkataba wa kuisadi wa Richmond/Dowans.

Uchunguzi wa gazeti hili umethibitisha kuwa Rostam aligawa fedha nyingi kwa baadhi ya wabunge, hasa wa viti maalum(Majina tunayo) ili wampigie makofi ya nguvu wakati wa kusasilisha maelezo yake.

Kuna madai pia kuwa aligawa fehda nzuri kwa baadhi ya waandishi wa habari (Majina tunayo) ili kuipunguza makali ripoti ya kamati teule.

Pamoja na jitihada zote hizo, bado zaidi ya asilimia 95% ya wabunge wanaiunga mkono kamati teule na wangetaka wahusika wote katika kashfa ya Richmond wachukuliwe hatua kali.

"Hawa watu hawajui kusoma mood ya wabung. wengi tuna hasira nae; tungemchanachana baada ya kuwasilisha utumbo wake, sauti za viti malum zingemezwa na sauti za wabunge wazalendo" amesema mbunge kijana na machachari.

Alipoulizwa Dk. Mwakyembe kama kweli kamati yake ilikuwa na ushahidi wa ziada unaoonesha Rostam ndiye Richmond/Dowans, alisema kwa ufupi " Tumuombee tu mwenzetu aruhusiwe kutoa dukuduka lake. Tutakayoyasema yatajulikana palepale ulingoni"
__________________

No comments: