Survival Sisters wako tayari
Kwa Utambulisho..
Walipokuwa wanaingia kwenye‘game’walikuwa wanajiita ‘Choka Mbaya Sisters’,wakafanikiwa kutoka na albamu yao ya kwanza iliyokuwa na jina la ‘Yatima’,lakini kunako mauzo wakala za uso na kuambulia jina kidogo tu,Mariam Mndeme anashuka nayo zaidi. Sasa wanajiita ‘Survival Sisters’,huku mkononi wakiwa na albamu ya pili waliyoipa jina la ‘Tukiwezeshwa Tunaweza’.Nawazungumzia mabinti watatu,Irene Malekela,Lucy Samsoni na Latifah Abdallah wanaoonekana pichani ambao wamesema na ShowBiz kwamba,sasa wako tayari kwa utambulisho wa albamu hiyo utakaofanyika Agosti 26,ndani ya ukumbi wa Dar West Park,uliyopo Tabata,Dar es Salaam.
Zaidi wasanii hao wenye ulemavu wa viuongo ambao hivi sasa wanafanya vyema kupitia ngoma yao yenye jina la ‘Siyo siri’,iliyomshirikisha Dully Sykes,walisema kwamba mastaa kibao wa Bongo Flava wamejitolea kuwapiga tafu siku hiyo,wakiwemo Profesa Jay,Fid Q,Dully na Mr.Blu na wengine kibao.
”Siyo wasanii hao tu, pia makampuni na watu binafsi wamejitolea kutusaidia kama Global Publishers,Morgan Sound,Dotnata Decorations, Screen Masters na Times FM.Habari hii na Mdau Abdallah Mrisho Salawi
No comments:
Post a Comment