Thursday, May 8, 2008

Watwangana Kisa Jaketi la Senti50 !!!


Vijana watatu ambao majina yao hayakuweza kufahamika mara moja, hivi karibuni walipigania Jaketi la Mwanamuziki, Curtis Jackson ‘Senti 50’ na kusababisha vurugu zilizowalazimu polisi kuwakamata.Senti 50 alitua nchini Jumapili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. JK Nyerere ambapo akiwa anatoka nje ya uwanja huo alivua jaketi alilokuwa amevaa na kuwarushia mashabiki wake waliofika kumlaki.
Subiri ni kudokeze ilivyokuwa Senti 50 akiwa anatoka nje ya uwanja huo alivua jaketi alilokuwa amevaa na kuwarushia mashabiki wake waliofika kumlaki.

Kufuatia kitendo hicho watu kadhaa walianza kugombea jaketi hilo na kusababisha vurugu kubwa baina ya vijana watatu waliokuwa waking’ang’ania jaketi hilo walilofanikiwa kulitia mikononi baada ya kuwashinda nguvu wenzao.

Hata hivyo, licha ya vijana hao kubaki watatu katika purukushani hilo walishindwa kuelewana na kuanza kutwangana ngumi kitendo kilichosababisha polisi wa uwanjani hapo kuwakamata.

“Wabongo bwana, sasa watu wamebaki watatu na jaketi mkononi wanashindwa kuelewana wanaamua kutwangana ngumi.
“Haya kiko wapi? Sasa wamekamatwa wanapelekwa kituoni na wakishangaa watasikilizia kwenye bomba onesho la senti50 na jaketi lenyewe wamelikosa ,” alisikika shabiki mmoja wa msanii huyo aliyefika kiwanjani hapo kumpokea senti50.

No comments: