Tuesday, May 6, 2008
Jinsi ilivyokuwa hadi anakitowa kutoka katika shooo Senti50 !!!!
Baada ya hapo senti 50 (50cent) na wana wa Gunit akatambaa kwenye mchuma huo pichani na mchezo ukawa umeishia hapo, kwa wale wenzangu na mimi waliodai ooh senti50(50cent) hawezi kuja
bongo,hakuna mwenye jeuri ya kumleta senti50(50cent) na maneno kibao ambayo kusema kweli yalikuwa hayana msingi wowote na pia kule ni kukosa kujiamini,kalaga baho kama ulifika kwenye shoo poa,kama hukufika ushahidi wa picha huo hapo na kimsingi habari ndio hiyo au sio
Yaani jamaa alikuwa pisi tu tofauti na baadhi ya watu walivyokuwa wakidhania, kwamba senti50 ana makuu kihivyooo,wenyewe tumejionea
Baada ya kumaliza shoo yake senti50 alipiga picha pamoja na baadhi ya wadau wa muziki wake kama hivi pichani
Wasanii wa kizazi kipya a.k.a bongofleva mpooo!mnalo la kujifunza kutoka kwa wana Gunit? hasa wale wana hip hop wenzagu,yaliyomo yalipatikana?
Wageni wetu nao pia walikuwapo fuluu
kwani tumibiishaaa wajameni.!
Lloyd Bank stejini
haa haa haaaa,senti50 noma kweli mtu wangu
watu fuluu halafu shangwe na kujiachia kwa sana,senti50 tena weee!
Tony Yayo akikamua kisawa sawa jukwaani
Mashabiki wajiachia kwa namna ya pekee kabisa, Senti50 aliangusha ngoma kwa muda wa masaa mawili na ushehe hivi,lakini mchaka mchaka wake ulikuwa haufai kwa watoto ni wakubwa tu, wakati mwingine unajikuta unanesa nesa huku kijacho kinakutoka mikono hewani,wacha weee!kwa aliyekosa mmh
Senti50 akiendelea kuwasuuza mashabiki wake vilivyo
Makamuzi ya mtu mzima Senti50 na vijana wake Lloyd Bank na Tony Yayo yalikuwa si ya kitoto mtu wangu, pichani si unaona alivyokuwa akiwarusha mashabiki ambao mara kadhaa walijikuta wakipiga mayowe na miluzi kila wakati
Senti50(50cent) jukwaani usiku ndani ya ukumbi wa diamond jubilee
diamond palikuwa hapatoshi kusema ukweli, kwa wale waliokuwepo wanaweza wakazungumza
Senti50 (50cent) yeye alikuwa akikamua huku akinesa tu jukwaani, huku mashaiki wake wapigawa viliyo ukumbini humo,
Lloyd Bank nae aliwakuna wengi bila hiyana
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment