Burundi Yashinda Faidika Na BBC!
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Juni 27 2008
Burundi ilshinda Faidika na BBC 2008.
Ashura Kisesa, raia wa Burundi, mwenye umri wa miaka 24, ameshinda zawadi ya juu ya shindano lililoendeshwa na BBC Idhaa ya Kiswahili, la kutafuta kijana mwenye kipaji cha biashara, lijulikanalo kama Faidika na BBC. Waziri mkuu wa Uganda, Apolo Nsibambi alimkabidhi Bi Ashura tuzo maalum pamoja na hundi yenye thamani ya dola elfu tano za Marekani, ili aweze kuanzisha mradi wake wa kujenga vyoo vya kulipia, katika miji ya Afrika Mashariki na Kati.
Ashura Kisesa, msichana pekee aliyeingia kwenye fainali hizo, zilizorushwa moja kwa moja, kupitia BBC Idhaa ya Kiswahili na Televisheni ya UBC, aliwashinda vijana wengine wanne, kwa kuwashawishi majaji na jinsi atakavyotumia fedha za zawadi kuanzisha mradi wenye mafanikio na kunufaisha jamii inayomzunguka.
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Mkuu wa Uganda, Profesa Apolo Nsibambi alisema “ Wakati shindano hili likianzishwa mwaka jana, hawakuwepo wasichana katika fainali, hivyo natoa pongezi kwa Ashura. Natoa wito kwa BBC kuchukua hatua ithibati kuhimiza wanawake zaidi kuingia katika biashara. Hii ni jitihada nzuri ya BBC ya kusaidia vijana kuwa wabunifu na kuwafanya wawe waundaji wa nafasi za kazi, badala ya kuwa watafutaji kazi”
Ashura aliwasilisha wazo lake, mbele ya jopo la majaji, katika matangazo yaliyorushwa moja kwa moja. Majaji hao walivutiwa na jinsi Ashura alivyowasilisha mchanganuo wake, na jinsi alivyopangilia. Mara baada ya kushinda Ashura alisema “ Nimefurahi mno kushinda. Ukosefu wa vyoo katika miji ya Afrika Mashariki na Kati, ni tatizo kubwa, na ni imani yangu kuwa nitaweza kuleta mabadiliko kupitia wazo hili la biashara”.
Naye Meneja mradi wa Faidika na BBC, Salim Kikeke alisema “ Hakika Ashura anastahili ushindi. Wazo lake la kibiashara ni zuri, na litawanufaisha watu wengi wa Afrika Mashariki na Kati. Namtakia kila la kheri, na nina hakika, huu ni mwanzo tu wa maisha bora kwake”
Wengine waliongia katika fainali hiyo ya Faidika na BBC ni Witness Omoga (22) kutoka Kenya, Rangira Aime Frederick (17) kutoka Rwanda, Apolinary Joseph Laksh (23) kutoka Tanzania, na Derrick Kajukano kutoka Uganda. Vijana hao watakuwa na nafasi ya kupata ushauri kutoka BBC watakapotaka kuanzisha biashara zao. Jopo la majaji liliundwa na Farijala Baraza Sadi kutoka Burundi, Mutagoma Madina kutoka Rwanda, Arnold Kweka kutoka Tanzania, John Ndungu kutoka Kenya na Jasmine Nakayima Adam kutoka Uganda.
Mbali na matangazo hayo ya moja kwa moja kurushwa kupitia shirika la utangazaji la Uganda UBC, tuzo za washindi zilichongwa na msanii kutoka Uganda, Peter Oloya, huku burudani ya muziki ikiporomoshwa na mwimbaji, mshindi wa tuzo kadhaa, Maurice Kirya pia wa Uganda. Unaweza kuona na kusikika matangazo hayo tena, kupitia bbcswahili.com/faidika.
Kwa taarifa zaidi tafadhali wasiliana na.
Christine George, Assistant Publicist, BBC World Service +44(0) 207557 1142; christine.george@bbc.co.uk
Taarifa kwa wahariri.
Ashura Kisesa anaweza kupatikana kwa ajili ya mahojiano kwa namba hi ya simu: +257 79465253 au kwa barua pepe: ashurakiss@yahoo.fr. Picha za hafla hiyo zinaweza kupatikana.
BBC Idhaa ya Kiswahili ni Shirika la Utangazaji ambalo hutoa huduma zake kupitia radio na kwenye mtandao kwa wasikilizaji wanaozungumza Kiswahili barani Afrika na ulimwengu mzima kwa ujumla. Kipindi cha BBC cha asubuhi Amka na BBC hurushwa hewani saa 12.00 asubuhi saa za Afrika mashariki, na hukuletea habari za eneo zima na duniani, pamoja na muziki na habari mbalimbali za kijamii. Kipindi maarufu cha BBC cha habari na uchambuzi Dira ya Dunia huanza saa 12 na nusu jioni. Leo Afrika husikika saa tatu kasorobo Afrika Mashariki, na hukuletea habari mbalimbali zilizotokea barani Afrika kwa siku hiyo. Mtandao wa BBC kwa kiswahili unapatikana katika bbcswahili.com. Katika mtandao huu, unaweza kupata taarifa za maandishi, matangazo yetu, makala na uchambuzi wa habari za Afrika na dunia nzima. Pia katika mtandao huu utapata taarifa na matangazo ya kipindi maarufu cha Kimasomaso, ambacho hutoa elimu ya afya ya uzazi na kuchambua mila na desturi zinazozingira suala zima la uzazi. Kipindi hicho kilianzishwa na kitengo cha kimataifa cha BBC cha misaada - BBC World Service Trust.
BBC World Service - Idhaa ya Dunia, ni shirika la habari la kimataifa la utangazaji linalotoa huduma za matangazo kwa lugha 33 mbalimbali. Shirika hili linatumia njia kadhaa kuwafikia wasikilizaji wake milioni 183 ulimwenguni kote, kwa kupitia Masafa mafupi, masafa ya kati, FM, satellite na viunganishi. Vituo washirika vya radio vipatavyo 2,000 hupitisha matangazo ya BBC, huku vituo kadhaa vukirusha taarifa zake kupitia simu za mkononi na vifaa mbalimbali visivyotumia nyaya. Wavuti wa BBC unatoa habari mbalimbali kwa maandishi, sauti na video, na vilevile kutoa nafasi kwa wasikilizaji kushiriki moja kwa moja katika vipindi kufuatana na matukio ya duniani. Takriban watu milioni 700 huvinjari katika wavuti huu kwa mwezi, na hivyo kuvutia karibu watumiaji milioni 40 kwa mwezi. Kwa taarifa zaidi tembelea bbcworldservice.com. kufahamu zaidi kuhusu Idhaa ya Kiingereza ya BBC, au kujiandikisha kupata majarida ya kwenye mtandao tembelea bbcworldservice.com/schedules.

No comments:
Post a Comment