shukran kwa jk toka burundi, kenya na comoro
Burundi, Comoro na Kenya zamshukuru Rais Kikwete
Na Mwandishi Maalum,
NCHI tatu za Afrika zimetoa shukurani rasmi kwa Tanzania, na hasa kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, kwa mchango wake mkubwa katika kutatua migogoro ya kisiasa katika nchi hizo.
Shukurani hizo zilitolewa na nchi za Burundi, Comoro na Kenya wakati wa Kikao cha 11 cha Wakuu wa Nchi za Afrika kilichofanyika mwanzoni mwa wiki hii katika eneo la kitalii la Sharm El Sheikh, Sinai, Misri.
Nchi zote tatu zilieleza kuwa bila Tanzania na hasa bila kujihusisha moja kwa moja kwa Rais Kikwete katika migogoro ya nchi hiyo, ingezichukua nchi hizo muda mrefu zaidi kwa migogoro hiyo kuweza kutatuliwa.
Shukurani za nchi hizo zilitolewa wakati wakuu wa nchi za Afrika walipokuwa wanajadili hoja ya kuanzishwa kwa serikali ya Umoja wa Afrika, moja ya ajenda kuu za kikao hicho cha siku mbili kilichofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha International Congress Center cha Hoteli ya Maritim Peninsula kuanzia Jumatatu, Juni 30, 2008, mwaka huu.
Makamu wa Rais wa Burundi, Yves Sahinguvu aliuambia mkutano huo: “Sisi wa Burundi, tunamshukuru sana Rais Kikwete kwa juhudi zake za miaka mingi kuweza kusuluhisha mgogoro katika Burundi ambao umefikia mwisho wake kwa kuhakikisha kuwa viongozi wa chama cha FNL-PALIPHEHUTU wanarejea nyumbani karibuni.”
“Tanzania, na hasa Rais Kikwete, tokea alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje, imehangaika na mgogoro wa Burundi kuliko nchi nyingine yoyote. Tunawashukuru sana Watanzania kwa mchango wao wa kindugu sana,” alisema Makamu huyo wa Rais.
Rais Kikwete ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho, alimjibu Makamu huyo wa Rais wa Burundi, “Hakuna shaka kuwa nchi zote katika eneo letu la Afrika zimechangia katika kusuluhisha mgogoro wa Burundi, lakini tunapokea shukurani hizo kwa “mchango wetu mdogo na wa unyenyekevu” tuliotoa katika Burundi. Tanzania ilijihusisha na mgogoro wa Burundi kwa kiasi cha miaka 14.
Naye Rais Sambi wa Comoro alitoa shukurani kwa jumuia ya kimataifa, na hasa kwa Rais Kikwete na viongozi wa Sudan na Libya kwa kuweza kusaidia kutatua mgogoro wa kisiasa visiwani humo uliosababishwa na uasi wa Kanali Mohammed Bakari katika Kisiwa cha Anjouan.
“Natoa shukurani za pekee kabisa kwa Mheshimiwa Rais Kikwete wa Tanzania, Rais wa Sudan, Omar El Bashir na kiongozi wa Libya, Brother-Leader kwa kuliwezesha tatizo la Anjouan kufikia mwisho. Bila damu yao, tungekuwa bado tunakabiliwa na uasi, na kwa kweli natoa heshima kubwa kwa umoja wa bara letu, AU, kwa kupitisha uamuzi uliowawezesha viongozi hao watatu kumaliza tatizo la Anjouan.”
Naye Naibu Waziri Mkuu wa Kenya, Uhuru Kenyatta alitoa shukurani kwa Rais Kikwete, katibu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Dk, Kofi Annan; Rais Museveni wa Uganda, Umoja wa Afrika (AU) na Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) kwa kuchangia katika usuluhishi wa mgogoro wa Kenya mwishoni mwa mwaka uliopita na mwanzoni mwa mwaka huu.
“Kama mnavyojua, mazungumzo ya usuluhishi yalianza Januari 28, mwaka huu, chini ya usimamizi wa Mheshimiwa Kofi Annan na kwa kweli tunamshukuru sana kwa uvumilivu wake katika kufanikisha mazungumzo haya.”
Aliongeza: “Lakini kwa kweli Kofi Annan angelazimika kuhangaika sana bila mchango muhimu sana wa Mwenyekiti wa AU, Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania. Lakini pia lazima tuwashukuru watu wengine – Rais Museveni, aliyekuwa mwenyekiti wa EAC, na taasisi zetu za AU na EAC yenyewe, kwa kusaidia kurejesha hali ya amani na usalama katika Kenya.”

No comments:
Post a Comment