Friday, July 4, 2008

Mbunge wa Tegeta Michuzi akiwa na ndito na shukrani ya kuungwa mkono anuani mpya

Anabandika hii akiwa na ndito kule a-taun mahususi kwa kuwashukuru wadau wote wa globu yake ya jamii kwani wasiwasi wake ni kwamba wengi watapotea mtaa baada ya kubalika kwa anuani kwenda www.michuzi-blog ulikuwa ni wa bure.

vile vile kuna walioomba kujua kama email address yake nayo imebadilika. jibu ni hapana. email yake ni ile ile issamichuzi@gmail.com na anaendelea kupokea picha, salamu, msaada tutani na chochote chenye kuendeleza libeneke.

pia anashukuru kwa kupokelewa vyema mwana mpya wa globu hii ya jamii anayekwenda kwa jina la www.bongotyube.com ambaye kazi yake ni kuendeleza libeneke la video za aina mbalimbali. huko pia mdau unakaribishwa kujisajili na kuweka video zako bila kupitia kwake. fuata maelekezo nawe utafanikiwa tu.

Anamalizia kwa asanteni sana wadau wote kwa kuendelea kumuunga mkono. naye anawaahidi kutowaangusha hata siku moja. anasema kijiweni kwake ni habari na picha ni za leo leo tu, hakuna kungoja nini wala nini

Kutoka kwa Mr .Michuzi

No comments: