Jennifer Mgendi Kuwainua
Wazanzibari kwa Injili...
Mwanamuziki wa Injili nchini,Jennifer Mgendi ameiambia ShowBiz kwamba,anarajia kufanya ziara visiwani Zanzibar na kuwafunua wananchi wake kwa nyimbo takribani 20 za kumtukuza Mungu.Msanii huyo amesema kuwa, zoezi hilo litakalofanyika ndani ya Ukumbi wa Golf,pia litamshirikisha Bahati Bukuku ambaye naye anafanya vizuri katika sanaa hiyo. Jennifer ambaye hivi sasa anasikika zaidi na wimbo wenye jina la‘mchimba mashimo’ alitamka kwamba, mbali na tamasha hilo yupo mbioni kutoka na filamu yenye jina la ‘Teke la mama.Habari na Mdau Abdallah Mrisho Salawi
No comments:
Post a Comment