Friday, March 13, 2009

wavuvi haramu kizimbani dar leo
msafara wa magari ya polisi ukiwasili mahakama ya hakimu mkazi kisutu muda mfupi uliopita
watuhumiwa chini ya ulinzi mkali wa askari maalum wa kupambana na ujambazi
hapa hatumwi mtoto
wakiwa kizimbani tayari kusomewa mashitaka yao

kwa kuwa washitakiwa ni wengi (jumla wako 38) na wamechukua nafasi yote mahakamani, paparazi wanakula nao sahani moja kupitia madirishani. kuna wengine wamebaki melini na huenda mahakama ikahamia melini kwani meli hiyo inasemekana haitakiwi kuzimwa na ni wao tu wanaoweza kuendesha mitambo,
-----------------------------------
PS: Kijana aliyempiga kofi Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi naye ameletwa mahakamani hapo asubuhi hii na kusimama mbele ya hakimu mkazi Mh. Neema Chusi.
Baada ya kusomewa shtaka, mtuhumiwa alikiri kumshambulia aliyekuwa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi kwa kumpiga kofi shavu la kushoto Machi 10, 2009 katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar.
Mwendesha Mashtaka Monica Mboga (Wakili wa Serikali): Je Ni kweli ama si kweli?
Ibrahim Saidi a.k.a Sultan a.k.a Ustaadh: Ni kweli

No comments: