Wednesday, March 11, 2009

JK awapongeza mabaharia waliokamata meli ya uvuvi haramu
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi akimzawadia zana za jadi za kabila la kimasai kiongozi wa operesheni ya kumata meli haramu Keith Govender.
Meli ya maharamia wa uvuvi iliyo kamatwa katika pwani ya maji kina kirefu ya tanzania ikivua bila kibali na imekutwa na shehena ya samaki tani zaidi ya 70 elfu.

JK akipokea zawadi ya kapelo toka kwa kiongozi wa meli inayoendesha operesheni ya uvuvi haramu katika bahari ya hindi, Keith Govender, leo Ikulu, Dar, alipowapokea ili kuwapongeza mabaharia wa meli hiyo iliyofanikiwa kukamata meli moja haramu. meli hiyo ilikamatwa juzi katika eneo la ukanda wa bahari wa uchumi, ambako maharamia hao walipoona vyombo vya operesheni hiyo waliongeza mwendokasi wa meli yao na kukimbia, lakini hawakufanikiwa na kukamatwa baada ya kutishwa kwa silaha. Operesheni hii imefanikiwa kwa kushirikisha nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambzo ni Kenya, Msumbiji, Afrika Kusini na Namibia, ambazo zimetoa wataalamu wake na vifaa kusaidia kudhibiti wizi huu.
JK akimpongeza Nwabisa Lutshete, mwanamama pekee baharia aliye katika meli hiyo ya kusaka wavuvi haramu katika hafla ilofanyika leo ikulu, dar


No comments: