Wednesday, March 4, 2009

mjadala wa kocha marcio maximo; abaki ama aondoke?
kocha wa taifa stars marcio maximo toka brazil akiwa na wakongwe wa soka ambao toka shoto ni kipa james kisaka, kipa juma pondamali na beki athumani chama.
kwa heshima na taadhima globu ya yamii inaanzisha mjadala wa kumjadili kocha maximo kwa nia ya kupata mawazo ya wengi baada ya kutolewa katika michuano ya CHAN kule ivory coast majuzi ambayo ndiyo ilikuwa ni kipimo tosha cha uwezo wake katika muda wa miaka miwili ya mkataba wake.
1. je, maximo amefanya kile alichokuja kukifanya?
2. mwezi julai mkataba wake unamalizika, je aongezewe ama aondoke?
3. kuna haja ya kuwa na kocha wa nje ama tubaki na wazalendo?

wakati ni kweli globu ya inawezekana inakaribisha maoni ya aina yoyote kuhusiana na mstakabali wa maendeleo ya soka nchini, si uwongo kwamba maoni yatayochafua hali ya hewa hayafai na hayatoona mwanga wa jua. hivyo mdau unaombwa utoe maoni bila jazba ama kashfa ili tujenge badala ya kubomoa.

-Kadidi2


No comments: