Wednesday, March 4, 2009

msiba ITV: Rehema Mwakangale hatunaye tena
Mtangazaji wa ITV Rehema Mwakangale (kulia) ametutoka jana asubuhi katika hospital ya Mikocheni alikokuwa amelazwa. Kwa Mujibu wa taarifa kupitia Radio One, mipango ya mazishi itakuwa kwa bibi yake Sinza karibu na Deluxe bar. Mola ailaze roho ya marehemu peponi
AMINA
Pichani ni marehemu Rehema Mwakangale akimhoji mama wa mtoto Samuel Nkya aliyeharibika sura na kupelekwa India kwa matibabu. Rehema alikuwa mstari wa mbele kufuatilia matibabu ya mtoto huyo ambapo globu ya jamii ikishirikiana na ITV viliweza kuchangisha pesa kufanikisha hayo matibabu. Picha zaidi BOFYA HAPA

No comments: