Tuesday, March 17, 2009

msondo ngoma inatisha!
safu ya waimbaji ya msondo ngoma. toka shoto ni kifaa kipya salim sultani a.k.a musemba wa minyigu, papa upanga na juma katundu. bendi hii inasifika pia kama chuo cha mafunzo kwani pamoja na ukongwe wake hii ni bendi pekee yenye vija na wengi wanaopiga muziki wa kiutu uzima usioisha utamu. hii ni shoo katika bonanza la michezio na muziki la kila jumapili ambapo msondo hutumbuiza na twanga pepeta bure chini ya udhamini wa kilaji cha kilimanjaro lager
papaa saidi mabera ambaye ndiye kakamata mpini wa 'suti' ya msondo ngoma asilia. toka ajiunge na bendi hii mwaka 1973 wakati huo ikiwa juwata jazz band hadi leo yupo na hajawahi kuhama
salim sultani akiongozwa na kamanda muhidin maalim gurumo
hassani, mtoto wa marehemu TX moshi william, ameachana kabisa na mambo ya bong fleva na kujikita vyema kwenye msondo ngoma, akifuata nyayo za baba yake. kwa kweli anakuja juu kwa kasi sana.
mkongwe shaaban lendi (kati) akiwajibika na wenzie katiba seksheni ya midomo ya bata
shoo ya msondo inaongozwa mama nzawisa ambaye hana mpinzani kwa manjonjo ya jukwaani mama nzawisa akiwa kazini hataki mchezo
mama nzawisa akistua kijoti romanus mng'ande a.k.a romario pamoja na kupuliza mdomo wa bata pia ni repa mkali sana


Video za msondo






No comments: