mzee ruksa aliposhambuliwa jukwaani juzi
Habari ni kwamba mtuhumiwa Ibrahim Said Sultan maarufu kama (Ustaadh) aliyemshambulia Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi kwa kumpiga kofi wakati akitoa hotuba katika Baraza la Maulid katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar juzi atafikishwa mahakamani leo kujibu shtaka la kushambulia hadharani.
Kamanda wa mkoa maalumu wa kipolisi wa dar afande Selemani Kova amesema upelelezi wa tukio hilo unaendelea ikiwa ni pamoja na kupima afya na akili yake pia kujua kama mtuhumiwa ni mwanaharakati na kama alikula njama na watu wengine kufanya kitendo hicho.
Kamanda Kova ameongeza juwa mtuhumiwa amehojiwa na kueleza kuwa hakuwa na nia ya kumdhuru Rais Mstaafu huyo lakini kwa kuwa ni mtu maarufu na anapendwa na watu wengi aliona akimfanyia kituko hicho atakuwa amefikisha ujumbe wake ambapo kijana huyo anapinga waislamu na wakristo kushirikiana katika kusherehekea sikukuu zao.
Kijana huyo amesema pia kuwa hapendi viongozi wa dini kushawishi jamii kutumia kondom kwani kwa mujibu maelezo yake hiyo ni kahamasisha matendo maovu ya zinaa ambayo hayakubaliki kidini.
No comments:
Post a Comment