Wednesday, March 11, 2009

Hoja: TFF Wakwepa Jukumu na Kumwachia Maximo
Bw. Kadidi na wadau wa soka,
Nina maoni marefu ila naomba mnivumilie kwani nafikiri ninahitji kuwa objective kwenye hili. Naomba niwashirikishe ninyi pia kutafuta ufumbuzi wa pamoja.
Mimi ni mdau wa soka hapo Tanzania lakini kwa sasa niko hapa Ujerumani. Nimekuwa nikifuatilia maendeleo ya nchi yetu kwa ujumla, lakini soka kwa namna ya pekee.
Kwa ujumla, hali si nzuri kabisa kwenye nyanja nyingi - kuanzia uchumi na siasa zake hadi soka. Nikijikita kwenye mada yangu, nimekuwa nikifuatilia timu yetu ya Taifa kwa ukaribu na mabadiliko ndani ya TFF. Naweza kusema Maximo kama kocha amejitahidi.
Pia, kukua kwa kiwango cha soka nchini kinaweza kuwa kumesababishwa na yafuatayo:
1. mwamko mkubwa wa wadau,
2. jitihada za vilabu kujibadilisha,
3. nia ya wachezaji kupata exposure (hata tamaa ya kucheza nje),
4. kuongezeka kwa wachezaji ambao pia wamepitia shule,
5. kuongezeka kwa thamani ya wachezaji nje hivyo vituo vya kukuza wachezaji kuongezeka,
6. kuongezeka kwa udhamini (modern marketing strategy ya makampuni mengi), na
7. nia za serikali - kuanzia wakati wa Mkapa aliposafisha FAT na kujenga "Old Trafford" (New and modern Stadium) yetu hadi wakati huu wa Kikwete kumleta Maximo na ku-support timu moja kwa moja.
Wadau, tatizo langu ni kubadilika badilika kwa timu ya Taifa kila kukicha. Sababu kubwa inayotolewa na Maximo ni nidhamu, uzalendo na lengo la kuleta mafanikio. Lakini wakati huo huo tukipoteza michezo Maximo anasema sababu wachezaji hawana uzoefu na bado anawajenga.
Wadau tusisahau kuwa kikosi ambacho Maximo alienda nacho Brazil sio hiki sasa. Kile ambacho kilishiriki qualifiers za Afrika na World Cup kwa kiasi kikubwa si hiki.
Pia, kikosi kinachocheza mechi nyingi za kirafiki ambazo zinaigharimu TFF na sisi tunaoingia uwanjani kwa mechi zilizo kwenye FIFA calendar si hiki. Yaani, huwezi kusema marekebisho mangapi kayafanya kwenye kikosi hiki.
Kwa ujumla, Maximo hana timu ya Taifa ambayo anarekebisha kidogo labda sababu ya majeruhi na kuporomoka kwa kiwango kwa wachezaji. Kila siku ni kikosi kipya ila ikitokea mchezaji wa kikosi kilichopita kajumuishwa, basi hiyo ni bahati yake.
Wakati makocha wengine, mchezaji mpya akiitwa kikosini, basi ndiyo ana bahati. Kwa Maximo, ni kinyume chake. Kwa ufupi, hakuna wachezaji muhimu na permanent kwenye Taifa Stars. Si kama akina Ronadinho, Kaka, Adriano, Robinho kwa Brazil; Mesi, Tevez, Mascherano, Aguiero, Zaneti kwa Argentina; Terry, Ferdinand, Cole(s), Rooney, Gerrard, James kwa England, n.k.
Kwa hali hii tusitegemee kuona timu ikikuwa na kukomaa. Kwa Maximo kila siku ni kuzaa timu changa. Hatoi nafasi kwa timu kukua na kukomaa. Hii inasababisha wadau kuhisi kama anabahatisha na kutafuta visingizio (timu ikifanya vibaya) kwa wadau ili wa-sympathy nae kwa kuwa wachezaji ni vijana na hawana uzoefu.
Kwa kweli alikuwa na nafasi kubwa ya kufanikiwa kama kocha kutokana na mazingira mazuri ya soka la Tanzania kwa sasa (kama sababu zinavyoonesha hapo juu) katika ukanda wetu hapo. Kwa nini anabadili timu kila kukicha? Maximo anasema nidhamu, uzalendo na lengo la kupata mafanikio ni vigezo muhimu kwake. Mimi naungana nae mkono moja kwa moja kwenye hili.
Ila natofautiana nae namna ya kuyapima na kuya-manage hayo. Yeye kama kocha ndiye mzazi wa mchezaji. Hivyo, jukumu la kumlea mchezaji ni lake. Pia, kama mzazi unakuwa karibu na wachezaji ili wa-feel uzazi wako. Lakini haingii akilini kuona kila siku anawaacha wachezaji kisa nidhamu, kakosa uzalendo na hajitumi. Hiangii akilini akina Chuji, Bobani, Abdi Kassim, Maftah, Farouk ambao amekuwa nao kwa miaka kadhaa ingawa wakati mwingine ni On and Off wamekosa hizo sifa leo.
Hatujasahau ya akina Machuppa, Abdallah Juma, Admini Bantu, Mwaikimba, Kaseja, Costa, Mussa Kipao, nk. Hao wachezaji wanajuhudi kubwa na wanajituma na ni tegemeo kwenye vilabu vyao. Iweje kwake tu tena baada ya kuwa nao kwa nyakati tofauti tofauti?
Inawezekana kweli mchezaji akakosea (hata Ulaya na Brazil kwake hutokea sana tu) utaifa unawekwa mbele. Alitakiwa aongee na meneja na TFF. Pale TFF, akina Kayuni/Madadi/Mwalusako/Mziray ndio wanafaa kuitwa na kushughulikia hayo na si nafasi za kisiasa za akina Rais na Katibu.
Walitakiwa kumwita mchezaji ambaye Maximo anamuona ana kasoro za kinidhamu, wanaongea naye na ikiwezekana kumtafutia wanasaikolojia na hivyo kumrudisha kwenye mstari. Akina Stephen Mapunda waliambiwa hawatavaa tena jezi ya Taifa hadi Ndolanga aondoke madarakani.
Hii si nzuri kwa soka letu na haitafikia tukakua na kukomaa. Naamini tungekuwa na wachezaji wengi walianza wakati wa kwenda Brazil na kucheza mechi zote za kirafiki na mashindani ambayo Maximo amesimamia, wangekuwa na uzoefu wa kutosha na hata kule CHAN Ivory Coast tungefanya vizuri zaidi.
Pia asikilize ushauri wa wadau. Kwa sasa anajivunia Tegete na Ngasa ambao alikuwa amewapuuzia wakati wadau walikuwa wanamlilia awajumuishe Taifa Stars. Boban pia aliwekwa kando hadi wadau walipolalamika sana na mwenyewe alimkubali kwenye mechi zetu na Bukina Faso, Senegal, nk.
Abdi Kassim alifunga goli bora na la rekodi Uwanja mpya na mwenye uwezo wa kubadili mchezo leo hana nidhamu. Sasa anataka wachezaji gani? Si vizuri kusikiliza wadau lakini haingii akilini kuwa na mchezaji wa kiwango cha juu halafu humtumii kwa taifa - mfano wa hili pia ni Kaseja.
Naomba wadau tujadili hili na TFF na Maximo wapate ujumbe ili tuzidi kuboresha si timu tu bali mkakati mzima wa kukuza soka Tanzania. La sivyo tutakuwa tunapiga "mark-time" miaka nenda rudi.
Hakuna haja ya TFF na Maximo kuanza kujitetea na kutoa sababu za hapa na pale ku-justify what is happening now!!
Wakubali kujifunza (kwani wasifikiri wako 100% perfect) ili tupige hatua mbele.
There's always a room for improvement.
Ni mdau mwenzenu
Geoff. I. Mwambe
Mannheim,
Germany

No comments: