Wednesday, March 11, 2009

mzee ruksa ashambuliwa jukwaani
Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi akiwa kwenye mkesha wa Maulid katika viwanja vya Mnazi Mmoja usiku wa kuamkia leo. Kulia ni kaimu Mufti Sheikh Suleiman Gologosi.
Jioni hii mzee wetu mpendwa alikuwa mgeni rasmi katika Baraza la Maulidi katika ukumbi wa Diamond Jubilee hall jijini, na alipokuwa akihutubia alitokea mtu ambaye kila aliyekuwepo alidhani anataka kurekebisha kipaza sauti.
Kwa mastaajabu na mstuko wa wote alimshambulia Rais mstaafu na kabla hajaleta madhara walinzi shupavu wa Rais mstaafu walimdhibiti mtu huyo kwa kumpiga mtama na kumshikilia.
wakati tukienda mitamboni mtu huyo ambaye hajajulikana mara moja wala sababu iliyompelekea kufanya vile, alikuwa amepelekwa mzobemzobe kituo kitogo cha polisi cha daraja la salender kwa mahojiano. Alhaj Mwinyi hakudhurika.

No comments: