Saturday, March 28, 2009

Msaada tutani kwa Matibabu ya Ugonjwa wa mifupa India
mtoto lazaro akiuguzwa na mama yake jovina zacharia nyumbani kwao buguruni
sehemu ya mguu wa mtoto lazaro ambayo inazidi kuoza kwa kukosa matibabu

Jina : Lazaro William.

Umri : Miaka 13.

Anapoishi : Buguruni.

Shule anayosoma : Hekima Shule ya msingi, Darasa la sita.

Hospitali alizokwishatibiwa : MOI(Idara ya mifupa katika hospitali ya Taifa Muhimbili), Bugando Mwanza, Nkinga Tabora, Burere Hospital Kibaha for Bone and Joint Surgery.

Nambari ya Akaunti: William, Jovina Zacharia, NMB(House Branch) Bank Ltd, A/c No.2231603793.

Mawasiliano : Unaweza kuwasiliana na Mama wa mtoto na pia kuongea na mtoto 0752 191296.

Barua pepe : tmajaliwa@yahoo.com.

Maelezo ya ziada:

Mtoto huyu alianza kuumwa kuanzia mwaka 2000 mwezi Julai.

MOI walisema kuwa akifika umri wa miaka 18 tatizo litakwisha,lakini hadi sasa hali ni mbaya sana.

Burere Hospital Kibaha Dr. alisema kama akishindwa yeye kumtibu hadi kupona basi itabidi apelekwe India kwa matibabu zaidi, mwaka jana Dr alishindwa akashauri mtoto apelekwe India.

Dr. Arab wa Hospitali ya Appollo tawi la Dar es salaam ameshauri mgonjwa apelekwe India kwa matibabu zaidi. Ugonjwa unaomsumbua ni OSTEOMYELITIES.

UKWELI ANATESEKA SANA. Gharama zote zilizomuwezesha kutibiwa katika hospitali mbalimbali zilikuwa ni michango kutoka kwa wasamalia wema.

Mama yake mtoto huyu alitelekezwa na baba yake muda mrefu sana wakiwa Mwanza.

MUNGU AWABARIKI SANA.

No comments: