Saturday, March 28, 2009

Mahunda: Urais Hausomewi, Dj Kachukua Nchi!

"...ndugu zangu,uwaziri hausomewi..." Haya ni maneno ya Mh.Kikwete wakati akitangaza baraza la mawaziri mwaka 2005.Hata urais hausomewi.Ingawa kwa hapa kwetu inahitajika shahada yoyote(si mimi ndivyo ilivyo).
Huko Madagaska DJ amechukua nchi,nna imani ataweza kama wenyewe wamemtaka kwa utaratibu wao,UKIZINGATIA HAUSOMEWI..Imeletwa na Clarence Mahunda, Hale, Tanga.
mambo ya viriyala
Heshima kwako ,
Hongera kwa libeneke lako! Naomba unitundikie hiyo mandahari ya hapa Durban Beach kama mfano wa kuigwa na wazee wa jiji hapo Dar ili kumuunga mkono JK katika juhudi za kuwaamsha wazee hao wapendezeshe miji yao !!
Ahsante
Mdau Mhandisi,
Sauzi
Msaada tutani kwa Matibabu ya Ugonjwa wa mifupa India
mtoto lazaro akiuguzwa na mama yake jovina zacharia nyumbani kwao buguruni
sehemu ya mguu wa mtoto lazaro ambayo inazidi kuoza kwa kukosa matibabu

Jina : Lazaro William.

Umri : Miaka 13.

Anapoishi : Buguruni.

Shule anayosoma : Hekima Shule ya msingi, Darasa la sita.

Hospitali alizokwishatibiwa : MOI(Idara ya mifupa katika hospitali ya Taifa Muhimbili), Bugando Mwanza, Nkinga Tabora, Burere Hospital Kibaha for Bone and Joint Surgery.

Nambari ya Akaunti: William, Jovina Zacharia, NMB(House Branch) Bank Ltd, A/c No.2231603793.

Mawasiliano : Unaweza kuwasiliana na Mama wa mtoto na pia kuongea na mtoto 0752 191296.

Barua pepe : tmajaliwa@yahoo.com.

Maelezo ya ziada:

Mtoto huyu alianza kuumwa kuanzia mwaka 2000 mwezi Julai.

MOI walisema kuwa akifika umri wa miaka 18 tatizo litakwisha,lakini hadi sasa hali ni mbaya sana.

Burere Hospital Kibaha Dr. alisema kama akishindwa yeye kumtibu hadi kupona basi itabidi apelekwe India kwa matibabu zaidi, mwaka jana Dr alishindwa akashauri mtoto apelekwe India.

Dr. Arab wa Hospitali ya Appollo tawi la Dar es salaam ameshauri mgonjwa apelekwe India kwa matibabu zaidi. Ugonjwa unaomsumbua ni OSTEOMYELITIES.

UKWELI ANATESEKA SANA. Gharama zote zilizomuwezesha kutibiwa katika hospitali mbalimbali zilikuwa ni michango kutoka kwa wasamalia wema.

Mama yake mtoto huyu alitelekezwa na baba yake muda mrefu sana wakiwa Mwanza.

MUNGU AWABARIKI SANA.

umbea wa nathan mpangala
kwa katuni zaidi nenda:
www.nathankatuni.wordpress.com
kiingrishi cha wenzetu




gari linapodumbukia barabarani dar
wasamaria wema wakijaribu kulichoropoa gari lililodumbukia kwenye shimo karibu na hellenic club kutokana na vifuniko vya mifereji ya maji kukosekana. watu wengi wameumia na kuharibu mali zao kwa tatizo hili ambapo wakati wa mvua shimo hulioni unastukia pwaaa!



kp na Busara zake..
Mh. Chenge katika msukosuko wa ajali yake
Kamanda wa Trafiki Dar afande Mohamed Mpinga (shoto) na Naibu Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai afande Peter Kivuyo (kati) na Mbunge wa Bariadi Mashariki Mh. Andrew Chenge wakielekea sehemu iliyotokea ajali ambapo gari alilokuwa akiendesha Mh. Chenge liligongana na Bajaji Ijumaa alfajiri na kusababisha vifo vya abiria wasichana wawili.
Mh. Chenge akieleza ajali ilivyotokea

gari alilokuwa akiendesha Mh. Chenge
Bajaji iliyogongana na gari la Mh. Chenge

Kwa habari kamili

Thursday, March 19, 2009

Hakuna Kwenda Mbele, Nyuma, Kulia Na Kushoto

Hapo kuna kugongana na kumalizana pia, hakuna kumsubiri wala kwenda kituo cha trafiki. Mnazi Mmoja, Dar, jana mchana.

Wednesday, March 18, 2009

mallya wa chacha wange ala mvua 3
Deus Mallya akipelekwa kuanza kutumikia kifungo leo huko Dodoma

Kijana Deus Mallya (27) aliyekuwamo kwenye gari lililopata ajali na kusababisha kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu baada ya kupatikana na hatia ya kuendesha gari kwa mwendo kasi.

Hukumu hiyo iliyotolewa leo, ilimfanya wakili aliyekuwa akimtetea, Godfrey Wasonga, kulia mahakamani hapo na kusababisha shughuli za mahakama kusimama kwa sekunde kadhaa.

Wakili huyo alilia baada ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mkoa wa Dodoma, Thomas Simba, kusoma vifungu vya kumtia hatiani mteja wake ambaye licha ya kuendesha kwa mwendo kasi, alihukumiwa kwa kuendesha gari bila leseni.

Hata baada ya hakimu kumaliza kusoma vifungu na kumtaka wakili atoe utetezi kabla ya hukumu, Wasonga alifanya hivyo huku akilia. Katika hukumu yake, Hakimu Simba alisema ameridhika na ushahidi wa upande wa mashitaka ambao ulitolewa mahakamani hapo.

Hakimu alisema makosa aliyobainika kuyafanya Mallya, yana adhabu kali, lakini alimpunguzia kutokana na ombi la mshitakiwa. Katika kosa la kuendesha gari kwa mwendo kasi na kusababisha kifo, alisema kwa mujibu wa sheria namba 63 kifungu cha pili (A) adhabu yake ni kifungo cha miaka mitatu jela.

Alimhukumu pia kwenda jela mwaka mmoja kwa kosa la kuendesha gari bila leseni na kusema kwamba adhabu zote zinakwenda pamoja. Kwa mujibu wa hakimu, kifo cha Wangwe kilisababishwa na kubanwa mlango wa gari wakati wa ajali na kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa na shahidi upande wa mashitaka namba nne, tano na sita, inaonyesha dhahiri mshitakiwa huyo aliendesha gari licha ya yeye kukana mashitaka hayo.

Hata hivyo, kabla ya hukumu kutolewa, Wakili Wasonga aliiomba mahakama itoe adhabu ya faini kwa mteja wake ombi ambalo lilitupiliwa mbali na mahakama. Awali, akijitetea kabla ya hukumu, Mallya aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwa kile alichodai kuwa ana wazazi wanaomtegemea.

Vilevile alidai kwamba anasomesha yatima na kwamba wapo vijana anaowasaidia kutokana na biashara zake na anamsomesha mdogo wake pia. Akizungumza baada ya hukumu nje ya mahakama, Wakili Wasonga alisema hajawa na uamuzi wa kukata rufaa hadi hapo atakapokaa na mteja wake (Mallya).

Ajali hiyo iliyosababisha kifo cha Wangwe na hatimaye kusababisha kijana huyo afungwe, ilitokea Julai 28 mwaka jana saa 2.30 usiku katika eneo la Pandambili, wilayani Kongwa takribani umbali wa kilometa 120 kutoka Dodoma.

Wangwe alikuwa akitoka Dodoma kwenda Dar es Salaam ambako pamoja na masuala mengine, alikuwa akienda kuhudhuria mazishi ya mwanasiasa mkongwe, Bhoke Munanka.

Ajali hiyo ilizusha utata mkubwa baada ya familia ya Wangwe kudai kwamba ndugu yao aliuawa na hivyo kulazimu waite madaktari kufanya uchunguzi kabla ya kuzikwa nyumbani kwake, Kemakorere, Tarime mkoani Mara.

Mbunge aliyechukua nafasi yake ni Charles Mwera.

Mahojiano ya Nakaaya na CNN Inside Africa

Mwanamuziki Nakaaya Sumari jana alionekana kwenye kipindi cha CNN Inside Africa, si kitu kigeni lakini kwa wanamuziki tena muziki wa Kizazi kipya ambao ulianza kwa kutokukubalika haya ni mafanikio makubwa sana kisanaa na kisanii pia.Nakayaa aliongea nini au alihojiwa nini?Nenda Spoti na Starehe upate kujua

VODACOM DAR INTERNATIONAL MARATHON YAJA MWEZI JUNI
NAIBU WAZIRI WA HABARI,MICHEZO NA UTAMADUNI,JOEL BENDERA(KULIA)AKIONGEA NA VYOMBO VYA HABARI JUU YA UZINDUZI WA VODACOM DAR MARATHONI ITAYOFANYIKA JIJINI JUNI 21, 2009 NA KILA MWAKA BAADA YA HAPO. (KATIKATI)MKUU WA UDHAMINI NA MAWASILIANO WA VODACOM TANZANIA,GEORGE RWEHUMBIZA,(KUSHOTO)MKURUGENZI WA MASOKO WA VODACOM TANZANIA EPHRAIM MAFURU
NAIBU WAZIRI WA HABARI,MICHEZO NA UTAMADUNI,JOEL BENDERA NA MKUU WA UDHAMINI NA MAWASILIANO WA VODACOM TANZANIA,GEORGE RWEHUMBIZA,WA PILI KUTOKA KULIA WAKISHIKILIA BANGO KUONYESHA INSHARA YA UZINDUZI WA MBIO ZITAKAZOJULIKANA KAMA VODACOM DAR MARATHON,(KULIA)KATIBU MKUU WA CHAMA CHA RIADHA TANZANIA SUILEMAN NYAMBUI,(KUSHOTO)MKURUGENZI WA MASOKO WA VODACOM TANZANIA EPHRAIM MAFURU
JK akutana na Raila Odinga London
JK akisalimiana na Waziri Mkuu wa Kenya Mh. Raila Odinga walipokutana kwa mazungumzo jijini London. Wote walialikwa na serikali ya Uingereza katika mkutano maalumu wa Afrika na mataifa makubwa kabla ya mkutano wa G-20
mama kikwete aasa wanaume wa kikurya dhidi ya kupiga mai waifu wao
Mama salma kikwete
Na Anna Nkinda wa Maelezo


Mama Salma Kikwete amewataka wanaume wa mkoa wa Mara kuacha tabia ya kuwapiga wake zao bali wawasaidie kufanya mambo ya maendeleo ambayo yatawasaidia kujikwamua kimaisha.

Mama Kikwete aliyasema hayo jana wakati akifungua semina ya siku mbili ya uwekezaji na ujasiriamali iliyofanyika katika ukumbi wa uwekezaji uliopo mjini Musoma.

“Nilikuwa nasikia kuwa eti wanawake wa mkoa huu wakipigwa na wanaume zao ndiyo wanaonekana kuwa wanapendwa sana sasa sijui kama ni kweli au la, lakini kwa kuwa leo niko na nyinyi wenyeji wa Mara nitajua kama ni kweli ”, alisema.
"Tatizo langu mie kwa watani zangu hawa ni hapo, je kinamama si wataona waume zao hawawapendi?
"Nasikia eti ikipita wiki bila kupigwa mama wa kikulya huanzisha zogo mwenyewe na asipopata kichapo basi atarusha jiwe juu ya bati afu atakinga mgongo iliaangukiwe nalo ndo amani inarejea ndani ya nyumba, kweli hayo watani???", alihoji.
Mama Kikwete pia aliwataka wakazi hao kuachana na imani za kishirikina za kuamini kuwa ukiwaua walemavu wa ngozi (albino) utapata utajiri na kuwataka kuwafichua wauaji wa albino.
“Kila mtu ana haki ya kuishi kama mwingine si vyema kuwafanya albino hawana haki ya kuishi na kuwaua pasipo sababu”.
“Acheni kuua albino kwani utajiri hauji kwa kuuza viungo vyao bali kwa kufanya kazi kwa bidii na kijituma kwa kufanya hivyo mtafanikiwa na kuondokana na umaskini”, alisema.
BONGO STAR SEARCH TABORA YAFANA

mamia ya washiriki wakiwa kwenye foleni ya kujiandikisha tayari kwa usaili
Kutoka kushoto majaji Master J, P-Funk and Elihuruma Ngowi wakiwa klabu ya Voice of Tabora (zamani Klabu Rufita) kwenye radio ya Voice of Tabora (VOT) FM 89.0 wakiongelea kuhusu BSS Tabora 2009.

Washindi wa BSS Tabora (wenye T-shirt nyeupe) kutoka kushoto: Shaban Mrisho, Leah Julius, Rajab Miraj na Kayombe Khamis wakiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja Huduma na Bidhaa wa Vodacom, Elihuruma Ngowi (kati) mara baada ya kutangazwa kuwa washindi Jumapili, Mach 15, 2009.
KILIMANJARO PREMIUM LAGER TANZANIA MUSIC AWARDS 2009
meneja wa kilaji cha kilimanjaro lager oscar shellukindo (kati) akionesha tuzo watazopata washindi wa kili music award 2008 hivi karibuni. kulia ni Dj John Dillinga a.k.a DJ JD na shoto ni afisa toka baraza la sanaa, Mzee Luhala. Hii ilikuwa mchana huu jijini Dar na chini ni orodha ya walioteuliwa kugombea nafasi katika kinyang'anyiro hicho cha kila mwaka kilicho chini ya udhamini wa kilimanjaro premium lager

MWIMBAJI BORA WA KIKE
VUMILIA
LADY JAYDEE
MWASITI
KEISHA
ISHA RAMADHANI
MWIMBAJI BORA WA KIUME
MATONYA
MAKAMUA
M. B. DOGG
HAMMER Q
Q. JAY
ALBAMU BORA YA TARAAB
V. I.P – Jahazi Modern Tarab
WHY – T. O. T
MWANAMKE HULKA - East Africa Melody
KITU MAPENZI - Dar ModernTaraab
WIMBO BORA WA TARAAB
(a) V. I .P Jahazi Modern Taraab

WHY – T. O. T
MWANAMKE HULKA - East African Melody
MWANAMKE MVUTO New Zanzibar Taraab
YA WENZENU MIDOMONI - Jahazi Modern Taraab
WIMBO WA MWAKA
TABASAMU –Mr Blue ft Steve
ANITA - Matonya ft Lady Jaydee
DAR MPAKA MORO - T. M. K Family
V. I. P - Jahazi Modern Tarabu
NZELA - Banana Zoro & B. Band
WIMBO BORA WA KISWAHILI (Bendi)
(a) SUMU YA MAPENZI - African Stars

(b) HESHIMA KWA MWANMKE - FM Academia

(C) SUPU UMEITIA NAZI - D. D. C Mlimani Park

(d) SAFARI SIYO KIFO - Akudo Impact

(e) MKONO SHAVUNI - Vibration Sound

ALBAMU BORA YA KISWAHILI ( Bendi)
(a) PEKECHA PEKECHA - Akudo Impact

(b) NYUMBA YA URITHI - Double M. Sound

(c) ULIMWENGU - J. K. T Band

WIMBO BORA WA R ‘n’B
(a) NATAMANI - M.B Dogg

(b) NEILA - Tundaman

(c) ZAMU YANGU - Sarah

(d) NATAMANI - Q. Jay na Makamua ft Joslin

(e) USINIACHE - Spark ft Chid Benz

WIMBO BORA WA ASILI YA KITANZANIA
(a) DELA DELA - Che Mundugwao & Mbeya Arts

(b) KATAA UNYANYASAJI WA KIJINSIA - Maringo Group

(c) KWETU SEREMA UKEREWE - Maringo Group

(d) KAZI YA DUKANI - Dogo Mfaume

ALBAMU BORA YA ASILI YA KITANZANIA
(a) DELA DELA - Che Mundugwao & Mbega Arts

WIMBO BORA WA HIP HOP
(a) BADO NIPO NIPO - Mwana F. A

(b) NIPE DEAL - Mangwea ft Dark Master

( c) NGOMA ITAMBAE - Chid Benz

(d) SIMTOMSAHAU - Kigwema ft Marlaw

(e) NAKUITA NJOO - Prof Jay ft Nyashinsky

12.WIMBO BORA WA REGGAE / RAGGA

(a) TUTAONANA WABAYA - Q . Chief

(b) MAMA NEEMA - 20%

(C ) RIPOTI - Tunda man

(d) DUDE LA KIMATAIFA - Chege

(e) TAXI BUBU - Matonya

13.MSANII BORA WA RAP

MANGWEA
FID Q
CHIDI BENZ
MWANA F.A
WITNESS
14. WIMBO BORA WA AFRICA MASHARIKI

(a) SWEET LOVE - Wahu (Kenya)

(b) TI – CHI - Ken Raz (Kenya)

( c) ZUWENA - Wezzre (Uganda)

(d) SIRIMBA Ngoni ft Lady Jadee ( Uganda)

(e) SALARY - Nameless (Kenya)

15. MTUNZI BORA WA MUZIKI

(a) MZEE YUSUPH

(b) KARAMA LEGESU

(C) M. B DOGG

(d) LADY JADEE

MATONYA
16. MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO

(a) AMBROSS A.K.A DUNGA

(b) LAMAR

( c ) MARCO CHALI

HAMIE B
MAN WALTER
17. MWANDIKAJI BORA WA NYIMBO

(a) PROFESOR JAY

(b) MATONYA

(c ) MWANA F.A

(d) LADY JAYDEE


18. WIMBO BORA WA ZOUK

(a)NAOMBA UMWAMBIE - Kalunde Band

(b) AWENA - Kassim

( c) NALIVUA PENDO - Mwasiti

(d) KARIM - Ally Kibba

(e) LONELY - Q Jay


19. MTAYARISHAJI BORA WA VIDEO

(a) VISUAL LAB

(b) KALLAGHE PRODUCTION

( c) MAUJANJA SUPPLIER

(d) EMPTY SOULS

(e) OUTCOME PRODUCTION


20. WIMBO BORA WA KUSHIRIKIANA (kolabo)

(a) GOODBYE - Chege ft Q Chief

(b) ANITA - Matonya ft Lady Jaydee

(c) NATAMANI – Q, Jay, Makamua ft Joslin

(d) SINTOMSAHAU - Kigwema ft Marlaw

(e) NAKUITA NJOO –Prof Jay ft Nyashinsky