Wednesday, July 16, 2008

Ziara nchini Uingereza imenitoa
Matongotongo-Jaydee
Mwanamuziki Machachari nchi Tanzania Lady Jaydee(Kulia)akiwa katika picha ya pamoja na Mwanamuziki/Mwigizaji wa Sinema na Vichekesho nchini Marekani Will Smith walipokutana kwenye Tamasha la Kumpongeza Rais wa Zamani wa South Africa Mzee Nelson Mandela kwa kutimiza Miaka 90 lilofanyika nchini Uingereza hivi Karibuni..
Mwanamuziki Lady Jay Dee(Kulia)akiwa na ML Criss ambaye ni mtangazaji katika kituo cha Redio Nairobi.,Kwa wengi mnaokumbuka ML Criss Pia alishafanya kazi kwenye kituo cha Redio cha 88.4 Clouds Fm cha jijini Dar es Salaam
Mwanamuziki Lady Jay Dee(wa pili kushoto)akiwa na wanamuziki wa kundi la
The Sugababes nchini Uingereza hivi Karibuni..
-------------
TAMASHA la 'birthday' ya kutimiza miaka 90 tangu kuzaliwa kwa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, lilifanyika Juni 27,mwaka huu katika viwanja vya Hyde Park jijini London,Uingereza.


Tamasha hilo lilihudhuriwa na watu mbalimbali mashuhuri duniani wakiwamo wanasiasa waliotoa mchango wao kuchangia Mfuko wa Nelson Mandela,ikiwa ni kumuenzi mshindi huyo wa Tuzo ya Amani ya Nobel kwa kutimiza umri wa miaka 90 baadaye mwaka huu.Tamasha hilo lilikuwa na lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kazi za jamii.

Tamasha hilo lilihudhuriwa na zaidi ya watu 46,664,namba aliyopewa kwa miaka 18 kati ya 27 aliyotumikia kifungo gerezani, na kulipambwa na sherehe zilizorindima kwa muziki na kushuhudiwa na zaidi ya watu bilioni 1 duniani.


Mfuko wa Nelson Mandela ulizinduliwa mwaka 2002,na kupewa jina la 46664,lengo likiwa ni kupambana na maradhi ya UKIMWI na kusaidia miradi ya taasisi za kupambana na maradhi hayo katika nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara.Mandela alifungwa jela mwaka 1964 kutokana na kuwa kiongozi aliyejihusisha na harakati za kupiga vita ubaguzi wa rangi Afrika Kusini. Aliachiwa huru mwaka 1991 na akawa Rais wa kwanza kuiongoza Afrika Kusini baada ya uchaguzi wa kidemokrasia kuanzia mwaka 1994-1999.

Katika tamasha la'birthday'ya Mandela mwaka huu,walikuwapo wasanii mbalimbali wa kimataifa,huku Tanzania ikiwakilishwa na Judith Wambura'Lady Jay Dee',aliyekwenda kwa udhamini wa Zain,ambayo ni Kampuni mama ya simu za mkononi ya Celtel Tanzania.

Tamasha hilo lililodhaminiwa na Zain Group,kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi inayoongoza Mashariki ya Kati na Afrika,lilimjumuisha pia Rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton.

Mbali ya Lady Jay Dee, pia walikuwapo wasanii wengine maarufu duniani kama Annie Lennox, Queen, Paul Rodgers,Simple Minds,Leona Lewis,Sugababes,Amy Winehouse, Razorlight,Johnny Clegg,Soweto Gospel Choir, Suzanna Owiyo,Dame Shirley Bassey.

Wengine ni Zucchero,Vusi Mahlasela,Emmanuel Jal,Sipho Mabuse,Josh Groban,Jamelia,Jivian Gasparayan, Amaral, Eddy Grant, Andrea na Sharon Corr, Children of Agape Choir, Jurt Darren, Loyiso, Joan Baez,Bebe Cool,Alif Naba,Hafiz, Maureen Lilanda, Emmerson Bockarie,Rogers Mpinganjira na D’Gary.


Pia mbali ya Lady Jay Dee,wasanii wengine waliodhaminiwa na Zain kwa lengo la kupromoti wasanii wa Afrika ni Alif Naba (Burkina Faso),Suzanna Owiyo (Kenya),D'Gary(Madagascar), Rogers Mpinganjira(Malawi),msanii wa hip-hop wa Nigeria,9ice,Emmerson Bockarie(Sierra Leone),Hafiz (Sudan),Bebe Cool(Uganda)na Maureen Lilanda(Zambia).

Mwingine aliyedhaminiwa na Zain ni Papa Wemba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambaye hata hivyo alishindwa kwenda London kutokana na kukosa viza ya kuingiza Uingereza, kwa mujibu wa Menaja Uhusiano wa Celtel Tanzania,Beatrice Mallya.


Lady Jay Dee alipangiwa kutumbuiza katika tamasha hilo kwa kuimba wimbo wa'Birthday Song' akishirikiana na Papa Wemba,lakini alishindwa kupanda jukwaani kutokana na mwanamuziki huyo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kukosa viza ya kuingia London.


Hata hivyo,Lady Jay Dee alipata wasaa wa kukutana na wasanii maarufu duniani wakiwamo Oprah Winfrey,Will Smith,Leona Lewis, Sugababes,Eddy Grant,Loyiso na Mandela mwenyewe."Nilipangiwa kutumbuiza kwa kushirikiana na Papa Wemba,lakini bahati mbaya alikosa viza ya kuingia London,hivyo nilishindwa kutumbuiza kwa vile mashairi ya wimbo alitunga yeye,na ratiba ilikuwa imepangwa,haikuwa rahisi kupanguliwa,"anasema Lady Jay Dee katika mahojiano maalumu Dar es Salaam baada ya kurejea nchini."Habari hii na Mwandishi Maalum

No comments: