Tuesday, July 15, 2008

Venezuela Wanyakua Taji la Miss
Universe 2008...
Miss Venezuela 2008 Dayana Mendoza akipungia wadau mbalimbali baada ya kutawazwa rasmi kuwa Miss Universe 2008 kwenye mashindano yaliyofanyika nchini Vietnam Usiku wa kuamkia jana.
Miss 2008 Elisa Najera, akiwa katika pozi mwanana na vazi lake jioni kwenye mashindano ya kumtafuta kimwana wa Miss Universe 2008
Miss Kosovo 2008 Zana Krasniqi,akiwa katika pozi na vazi lake la jioni..Kimwana huyu nae alitinga kwenye kumi bora za kuwania Taji la Miss Universe 2008 nchini Vietnam usiku wa kuamkia jana.
Miss Australia 2008 Laura Dundovic,akipita mbele ya majaji na vazi lake la jioni kwenye mashindano ya kumtafuta miss Universe 2008 kimwana huyu pia alitinga kumi bora.
Miss Spain 2008 Claudia Moro,akiwa katika pozi na vazi lake la jioni kwenye mashindano ya kumtafuta kimwana wa Miss Universe 2008 nchini Vietnam ambapo mwakilishi wetu kutoka Tanzania Amanda Ole sulul alishindwa kufurukuta.
Miss USA 2008 Crystle Stewart ambaye alifanikiwa kuingia katika kumi bora za mashindano hayo akiwa amekula pozi kati vazi lake la jioni Muda mfupi kabla hajadondoka ukumbini..hii ni mara ya pili mwa mshiriki kutoka nchini marekani kula mweleka kwenye mashindano kama haya.
Miss Colombia 2008 Taliana Vargas,ambaye pia alitinga kumi bora akiwa katika pozi mbele ya majaji na vazi lake la jioni kwenye mashindano ya kumtafuta kimwana wa Miss Universe 2008 nchini Vietnam usiku wa kuamkia jana.
Kumi Bora ya Vimwana waliyoshiriki shindano la kutafuta Miss Universe 2008 nchini Vietnam usiku wa kuamkia jana ambapo kimwana Dayana Mendoza alinyakua Taji hilo na nafasi ya tano kwenda kwa Miss Mexico,Nne Miss Russia,Tatu Jamhuri ya Domica na ya Pili Colombia..

No comments: