Wednesday, July 16, 2008

Nauli Za Mabasi Zazidi
Kupanda..
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA) Ezraeli Sekilasa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati akitangaza nauri mpya za daladala na mabasi ya mikoani.Picha na Mrocky.

-------------

Akitangaza viwango vipya kwa daladala zinazofanywa safari zake Dar es Salaam,Bw. Sekirasa alisema nauli ya njia fupi imepanda kutoka sh.250 hadi sh.300,njia za kati kutoka sh.300 hadi sh.400 na njia ndefu inayofikia umbali wa kilometa 25 itakuwa sh.sh.500 kwa safari moja.Bw. Sekirasa alisema njia ndefu inayofikia umbali wa kilometa 30 nauli itakuwa sh.600 kwa safari moja.

"Kwa upande wa Dar es Salaam nauli ya sh.300 ni kwa kupanda na kushuka ndani ya eneo lililo ndani ya barabara za Temeke,Mandela,Sam Nujoma na Mikocheni,"alisema Bw.Sekirasa.Mara baada ya nauli hiyo kuanza kutumika,eneo hilo litakuwa likiitwa Jiji Kati.Akizungumzia wanafunzi,alisema nauli yao pia imepanda kutoka sh.50 hadi sh.100.Alisema ifikapo Julai mosi mwakani nauli yao itapanda tena ambapo wataanza kulipa nusu nauli ya mtu mzima."Wakati ukifika,SUMATRA itatoa mwongozo ili kujua nusu nauli ya mtu mzima ni kiwango gani,kwani lengo letu ni kuinua ubora wa huduma na kupunguza visingizio vya kuonea wanafunzi," alisema Bw. Sekirasa.

Alisisitiza kuwa utekelezaji wa sheria ya nusu nauli kwa wanafunzi utategemea tabia na mwenendo wa wenye magari kuanzia sasa hadi ifikapo Julai mosi mwaka ujao.Akizungumzia kupanda kwa nauli ya wanafunzi,Bw.Sekirasa alisema;"Sio jambo dogo kupandisha nauli ya wanafunzi, lakini inabidi tufikie hatua tuendeleze sekta hii."Habari na Reuben Kagaruki

No comments: