Miss Tanzania EU 2008 ajiengua
Kwenye Miss Tanzania
2008..
Miss Tanzania EU 2008 -LUCY MWIZA FUNDIKIRA Pichani,amejitoa katika kinyang’anyiro cha Miss Tanzania 2008.Akizungumza na wanahabari Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Lino Agency waandazi wa Miss Tanzania Uncle Hashim Lundenga amesema kuwa walipata taarifa toka kwa muaandaaji wa shindano hilo EU kuwa Miss Fundikira hatoshiriki kwenye kinyang’anyiro hicho bila kusema kiundani sababu hasa za kufikia maamuzi hayo.Hata hivyo habari zaidi zinasema Miss Lucy ni mmoja wa mamiss wanne ambao hawatoshiriki kwenye kinyang’anyiro hicho.Mrembo namba mbili Kinondoni,Joan Faith pia amejitoa katika shindano na nafasi yake imechukuliwa na Miss Temeke namba nne Lilian Shayo baada ya warembo namba nne na tano wa kanda hiyo kushindwa kufika katika kambi hiyo,” alisema Lundenga.
No comments:
Post a Comment