Tuesday, July 15, 2008

Namshtaki Rostam Aziz amegushi
Saini si Yangu- Mch. Mtikila

Pichani ni Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP)Christopher Mtikila akionyesha gazeti la HabariLeo alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana..
-----------
Christopher Mtikila,amesema atamfungulia kesi mahakamani Mbunge wa Igunga,Rostam Aziz. Alidai mashitaka hayo yatakuwa ni pamoja na ya kughushi saini katika stakabadhi ya malipo anayodai alilipwa kama mkopo na si sadaka au mchango wa Kanisa kama inavyodaiwa.
Wakati Mtikila akiyasema hayo,suala la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kutangaza kutotambua mchango alioutoa Rostam alipoalikwa kwenye uzinduzi wa kwaya,limeleta changamoto mpya baada ya baadhi ya taasisi za dini kutaka zipewe namba ya mbunge huyo ili zimwalike azichangie fedha.
Mmoja wa Wainjilisti kutoka Huduma ya Biblia ni Jibu kutoka Morogoro,Damian Ndimbo aliomba apewe namba ya simu ya Rostam kwa lengo la kumpigia na kumwomba aipatie msaada wa kifedha taasisi yake. “….Mbunge Rostam Aziz kuchangia kanisa yupo sahihi,kwani kanisa limesababisha hayo yote na kama mna namba yake mnitumie aje asaidie na huduma yetu,”alisema Ndimbo kwa njia ya simu.Kwa habari zaidi Bofya na Endelea Hapa...>>>>

No comments: