Monday, July 21, 2008

Mradi wa Maji Safi Wilayani
Bukombe..
Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein,akimtwisha ndoo ya maji safi bibi Regina Mageni mkazi wa kijiji cha Bwerwa Wilayani Bukombe mara baada ya kuzindua mradi wa maji safi na salama katika kijiji hicho.
----------
Makamu wa Rais Dk.Ali Mohamed Shein,amezindua mradi wa maji safi na salama kwa wananchi wa kijiji cha Bwerwa Wilayani Bukombe wakati alipokuwa katika ziara yake ya kukagua na kuangalia miradi ya maendeleo Wilayani humo.

Jumla yashilingi milioni 51.7 zimetumika katika kukarabati mradi huo ambapo Makamu wa Rais ameahidi kuchangia shilingi milioni 1.5 kusaidia mfuko wa kikundikinachosimamia mradi huo.

No comments: